Naibu Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia
January Makamba akizungumza na watendaji wakuu wa kampuni ya Vodacom (hawapo pichani)
wakati alipotembelea makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es salaam katika
ziara maalum ya kujifunza shughuli za mawasiliano nchini. Kulia na Mkurugenzi
Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na
Teknolojia January Makamba akilakiwa na Mkuu wa Mahusiano na Mawasiliano wa
Vodacom Tanzania Joseline Kamuhanda. Makamba alitembelea makao makuu ya Vodacom
katika ziara ya kujifunza shughuli za kampuni hiyo. Katikati ni Meneja wa
Mahusiano ya Nje wa Vodacom Salum Mwalim.
Naibu
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia January Makamba na Mkurugenzi
Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza wakibadilishana uzoefu kabla ya Naibu
Waziri kufanya mazungumzo na watendaji wakuu wa Vodacom Tanzania alipofanya
ziara ya utambulisho makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es salaam.
Naibu
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi an Teknolojia January Makamba akikaribishwa
makao makuu ya Vodacom Tanzania na Ofisa Mkuu wa Mahusiano na Mauzo kwa Wateja
Wakubwa waVodacom Tanzania Mwamvita Makamba. Naibu Waziri Makamba alifanya
ziara ya utambulisho Vodacom na kukutana na Uongozi wa kampuni hiyo.
No comments:
Post a Comment