Pages

KAPIPI TV

Wednesday, May 23, 2012

MBUNGE WA SIKONGE SAID NKUMBA AWATAKA WANANCHI KUTOINGIZA SIASA KWENYE MIRADI YA MAENDELEO

 Mbunge wa jimbo la Sikonge Bw.Said Nkumba wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Makazi kata ya Ipole wilayani Sikonge mkoani Tabora.
Na Hastin Liumba,Sikonge
 
MBUNGE wa jimbo la Sikonge,mkoani Tabora,Said Nkumba,(CCM),amewataka
wananchi wa jimbo hilo kuacha tabia ya kuingiza siasa kwenye miradi ya
maendeleo inayotekelezwa na serikali.

Kauli hiyo aliitoa jana alipotembelea miradi ya maji safi na salama,na
shule ya sekondari Ugunda,iliyopo katika kijiji cha Makazi,kata ya
Ipole,wilayani humo.

Akiwa katika mradi wa maji,ulianzishwa mwaka juni 1, 1977,mradi ambao
umekuwa ulizinduliwa na  rais wa kwanza wa jamhuri ya muungano wa
Tanzania,hayati baba wa taifa Julius Nyerere,aliwaasa wananchi hao
kuacha mara moja kuingza siasa katika miradi ya maendeleo.

Aidha alisema amegundua kuwa katika kijiji hicho,kuna mambo ya siasa
katika kutekeleza miradi hususani mradi huo wa maji ambao umekuwa
ukigawa maji katika chemchem hiyo na kusambaza katika vijiji vya
Makazi,Ipole na Udongo.

Alisema miradi hiyo siyo ya CCM bali ni mali ya wananchi kamwe kusiwe
na visingizio vya propaganda za wachache wenye uchu wa madaraka.

Nkumba aliongeza kuwa licha ya mradi huo kuwa na changamoto
nyingi,bado wananchi wanatakiwa kuchangia fedha ili mradi huo uwe
endelevu.

Alisema bila ya kuchangia maji hayo hayataweza kupatikana na kamati
zote za kata zinzosimamia maji kusimamia mradi wa maji na kukabiliana
na changamoto zote ambapo yeye kama mbunge atashirikiana nao.

Nkumba alisema huduma ya maji haina siasa hvyo atasimamia miradi yote
ya maji iliyopo jimboni kwake kwa nguvu zote.

Hata hivyo aliwataka viongozi wa kata na vijiji kutojitenga katika
utendaji wa kazi za kila siku yeye kama mbunge atashirikiana nao
katika kuchagiza maendeleo na kuondoa kero zote zinzowakabili
wananchi..

Mbunge huyo katika ziara yake jimbo humo,alitembelea shule ya
sekondari Ugunda,na kujionea ujenzi wa chumba cha darasa kimoja
kitakachogharimu kiasi cha sh milioni 2,953,000.

Mkuu wa shule ya Sekondari Ugunda,Merina Mbiha,akisoma taarifa yake
alisema licha ya ujenzi wa chumba kimoja cha darasa kitakachogharimu
sh milioni 2,953,000,pia kuna nyumba ya mwali moja inayojengwa na
itagharimu sh milioni  21,400,000.

Alisema kati ya fedha hizo kiasi cha sh milioni 4,000,000 ni michango
na nguvu kazi za wananchi wa kata hiyo.

Aidha mkuu huyo wa shule ya sekondari Ugunda,alisema shule hiyo ina
wanafunzi 259 ikiwa na wavulana 134 na wasichana 125.

No comments: