Makamu Mwenyekiti wa JUWASAWINGO Bw.Onesmo Ole Ngurumwa akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari
MKUTANO NA VYOMBO VYA HABARI- UBUNGO PLAZA 27 MEI, 2012
UMUHIMU WA BARABARA YA MTOWAMBU-LOLIONDO/MUGUMU-MAKUTANO KWA WANANCHI
WA WILAYA YA NGORONGORO NA TANZANIA
JUWASAWINGO ni umoja
wa watu wa Wilaya ya Ngorongoro, waliojitoa kutetea maslahi ya jamii
ya wanangorongo ambao wamekuwa pembezoni kimaendeleo kwa miaka mingi. Jukwaa hili
huwaunganisha wanangorongoro wenye taaluma
mbalimbali kama wanachama ambao kwa sasa wanafikia 2000. Na wanachama wa Jukwaa
hili wanatoka vijiji vyote vya Wilaya Ngorongoro.
Kutokana na kuguswa sana na suala zima la ujenzi wa
barabara ya lami inayounganisha mikoa ya Arusha na Mara, Wana-JUWASAWINGO wanapenda kuweka wazi maoni
na msimamo wa Wananchi wa Wilaya ya
Ngorongoro juu ya suala hilo.
JUWASAWINGO imetambua kuwa kwa miaka mingi sasa, serikali
yetu imekuwa na nia nzuri ya kujenga barabara ya Mtowambu-Loliondo/Mugumu
Makutano ambayo itawanufaisha wakazi wa Wilaya za Ngorongoro, Monduli, Longido , Serengeti na Tanzania kwa ujumla.
Tunaamini kwa dhati kuwa upinzani wowote juu ya ujenzi wa barabara hiyo, uwe unatoka kwa nje ya nchi au ndani, kwa
watu binafsi au vikundi vya watu,
unapingana na matakwa ya wananchi wa Wilaya ya Ngorongoro.Wapinzani hawana,
hawajui au wameamua kuupuuza ukweli wa mambo juu ya mradi huo wa barabara.
Serikali imekuwa ikifikiria kuijenga barabara
hiyo tangia miaka ya mwanzo ya 1980. Katika
miaka ya karibuni, serikali iliibua upya kusudio lake hilo na ikaamua kuendelea
na utekelezaji wa mpango wa ujenzi huo uliowekwa pembeni kwa siku nyingi.
Wapinzani wa mpango huu wamekuwa wakijifanya
kuifahamu jiografia ya eneo hili la nchi yetu kuliko wenyeji na wamekuwa
wakitumia mbinu mbalimbali ili kuungwa mkono na jamii ya kimataifa ikiwemo
mbinu ya kuibatiza kimakosa barabara hiyo na kuiita”Barabara Kuu ya Serengeti”
au kwa Kiingereza “Serengeti Super
Highway”!
No comments:
Post a Comment