Pages

KAPIPI TV

Wednesday, May 30, 2012

CHAMA CHA WANASHERIA WANAWAKE TAWLA CHAWAPA SOMO WANAHABARI KUHUSU MABADILIKO YA KATIBA NA HAKI YA AFYA YA UZAZI

Wakili Bernadetha Mkandya ambaye pia ni mwanachama wa Chama cha Wanasheria wanawake TAWLA akizungumza katika semina ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali iliyoandaliwa na TAWLA inayozungumzia Mabadiliko ya Katiba na haki ya Afya ya Uzazi inayofanyika kwenye Hoteli ya Blue Pear Ubungo Plaza jijini Dar es salaam.

Moja ya mada zilizochukuwa muda mrefu kujadiliwa ni kuwa katiba mpya izungumze wazi kwamba haki ya mtoto wa kike atambulike kuwa ni mtu mzima akiwa na miaka 18 na pia izungumze wazi juu ya elimu ya mtoto wa kike, kuwa angalau apate elimu kufikia kidato cha nne.

Pia washiriki  wanapendelea kuwa katika katiba iundwe tume ya kushughulikia masuala ya jinsia ya Mwanamke na mwanaume.

Wakili Bernadetha Mkandya ambaye pia ni mwanachama wa Chama cha Wanasheria wanawake TAWLA aakifafanua jambo  katika semina hiyo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika semina hiyo kutoka kulia ni Martha kutoka TBC, Oscar Mbuza Habari Leo na Jane Mihanji Uhuru.

No comments: