Mganga mkuu mkoa wa Tabora Dr.Leslie Mhina akiwa ofisini kwake hospitali ya mkoa Tabora.
Mganga mkuu mkoa wa Tabora Dr.Leslie Mhina amewataka wanaume waishio mkoani Tabora ambao hawajafanyiwa tohara kufika katika vituo vilivyoandaliwa ili waweze kupata huduma hiyo inayotolewa bure.
Dr.Mhina ametoa rai hiyo wakati akiongea na mwandishi wetu ofisini kwake katika hospitali ya mkoa wa Tabora Kitete alipokuwa akielezea mafanikio na changamoto tangu kuanzishwa kwa mradi huo mkubwa wa Tohara kwa wanaume mkoani Tabora.
Akielezea changamoto zinazoukabili mradi huo wa Tohara,Dr Mhina alisema bado kuna idadi ndogo ya wananume mwenye umri kati ya miaka 16 hadi 35 wanaojitokeza kupatiwa huduma hiyo katika vituo vilivyopangwa.
"Moja ya lengo la kufanya tohara kwa wanaume ni kusaidia kuwaepusha kupata maambukizi ya ukimwi kwa wastani wa asilimia 60 wakati wakifanya tendo la ngono"alisema Dr.Mhina
Aliongeza kuwa idadi ndogo ya wanaume wa umri huo imekuwa nisehemu inayochelewesha lengo la kuwafikia rika ambalo linatajwa kuwa ndilo lililo katika hatari ya kupata maambukizi ya ukimwi
endapo kama hawajafanyiwa tohara.
Aidha kwa upande mwingine Dr.Mhina alisema hadi sasa Tohara imekwisha fanyika kwa asilimia 25 kwa wastani wa vituo sita kwa mkoa wa Tabora.
Sambamba na watoto chini ya umri wa miaka 15 ambao ndio wamejitokeza kufanyiwa tohara,Dr.Mhina amewataka wanaume kujitokeza kufanyiwa tohara huku akianisha kuwepo kwa taratibu za usiri mkubwa miongoni mwa watu watakaojitokeza kufanyiwa usafi huo.

No comments:
Post a Comment