Pages

KAPIPI TV

Monday, April 30, 2012

WAANDISHI WA HABARI SINGIDA WAPATA MAFUNZO HABARI ZA UCHUNGUZI

Baadhi ya waandishi wa habari mkoa wa Singida,wakifuatilia kwa makini mafunzo ya uandishi wa habari za uchunguzi yaliyokuwa yakitolewa na mwezeshaji Nyaronyo Kicheere.

Msimamizi wa mafunzo yanayohudhuriwa na baadhi ya waandishi wa habari Singida, Jackob Kambili kutoka UTPC,Mwanza,akisisitiza jambo wakati wa mafunzo.

Mwezeshaji wa mafunzo ya uandishi wa habari yanayohudhuriwa na waandishi wa habari mkoa wa Singida yanayohusu uandishi wa habari za uchunguzi,Nyaronyo Kicheere,akitumia ramani ya dunia katika kutoa mafunzo.
Baadhi ya waandishi wa habari wa mkoa wa Singida,waliohudhuria mafunzo ya uandishi wa habari za uchunguzi yaliyomalizika .Picha zote na Nathaniel Limu.
Nathaniel Limu Singida 
                                                                                                                             
KLABU ya waandishi wa habari (SINGPRESS) mkoani Singida. kwA kushirikiana na Umoja wa vilabu vya waandishi wa habari nchini (UTPG), kimeandaa mafunzo ya siku sita ya uandishi wa habari za uchunguzi kwa wanachama wake 10.
 
Mafunzo hayo yanafanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kanisa Katoliki mjini hapa.
 
Mwezashaji wa mafunzo hayo ni wakili wa kujitegemea Nyaronyo Kicheere na yanasimamiwa na Jackob Kambili kutoka UTPC, jijini  Mwanza.
 
Nyaronyo alitaja baadhi ya mada zitakazotolewa kuwa  ni pamoja na uelewa wa uandishi wa habari za uchunguzi, sifa za habari za uchunguzi na vyanzo vya habari za uchunguzi.
 
Akitoa mada zake, Nyaronyo aliwataka waandishi wa habari kwanza  kuhakikisha  wanakuwa na taarifa za uhakika na zilizojaa ukweli mtupu kabla hawajaandika habari za uchunguzi.
 
“Jihadharini sana na taarifa za uvumi, msifanyie kazi mambo ya uvumi, hakikisheni mnafanyia kazi taarifa zenye sifa, taarifa zinazoweza kuthibitishwa endapo itahitajika”,alifafanua Nyaronyo.
 
Aidha, aliwataka kufanya juhudi zaidi katika kutafiti taarifa za uchungi ili ziweze kukidha mahitaji.
 
“Muwe na tabia ya kukusanya taarifa muhimu na sahihi zinazokidhi malengo na pia muwe na  mbinu zitakazowawezesha kufanya  utafiti wa kina ili pamoja na mambo mengine,za kujua ukweli wa hicho unachokichunguza",alisema Nyaronyo na kuongeza;

"Mkifanya hivyo,habari mtakazozitoa zitaonyesha umahiri na uwezo wenu na kwa njia hiyo,mtakuwa mnajijengea heshima mbele ya jamii”,alisema.










No comments: