Mbunge Tundu Lissu akihutubia mkutano viwanja vya stendi ya zamani mjini Singida, tangu mahakama kuu impe ushindi dhidi ya kesi
Wafuasi na wapenzi wa CHADEMA wakiitikia kukunja ngumi juu kuonyesh nguvu ya umma katika mkutano huo, mbele ni mtoto Hilda Jack
Mbunge
wa Singida mashariki Tundu Lissu(wa pili kulia),akiingia kwenye viwanja
wa stendi ya zamani mjini Singida kwa ajili ya mkutano
Mbunge wa Singida mashariki Tundu Lissu akimtolea mfano muuza maji mjini Singida kwa kutumia toroli, maarufu kwa jina la 'Chai
Na Nathaniel Limu na Elisante John,Singida
CHAMA
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetoa wito kwa viongozi na
wanachama ‘safi’, walio ndani ya CCM, wajiunge mapema na CHADEMA ili
waikomboe nchi, kutoka kwa watu aliowaita wezi na mafisadi wanaokula fedha za umma.
Mnadhimu
mkuu, kambi ya upinzani bungeni, Tundu Lissu, alitoa rai hiyo kwenye
mkutano wa hadhara, aliofanya eneo la stendi ya zamani, mjini Singida,
kwa lengo la kukiimarisha chama, bada ya kushinda kesi yake ya uchaguzi dhidi ya makada wa CCM.
Lissu
ambaye pia ni mbunge Singida mashariki, aliwashauri wajiondoe mapema katika vyama walipo sasa,
badala ya kung’ang’ania huko, kusubiri CHADEMA itawale nchi, halafu
ndio wajitokeze kusema na wao ni wafuasi wa chama hicho.
Pia aliwaomba
viongozi, wanachama na wafuasi wa CHADEMA hivi sasa wachukue
tahadhari, vinginevyo watapata madhara makubwa, ikiwemo hata kupoteza
maisha yao kutokana na kuwepo kwa hujuma mbalimbali dhidi ya chama chao.
Alisema
kitendo cha kuuawa kwa mwenyekiti wao huko Usa river, mkoani Arusha na
kukatwa katwa kwa mapanga wabunge wa CHADEMA mkoani Mwanza, ni dalili mbaya kwa
wanachama na viongozi wa chama hicho dhidi ya maisha yao.
“Vita
hii ni kubwa, lazima tuielewe, kuanzia sasa kaeni chonjo, vinginevyo
CHADEMA tutauawa, mwenyekiti wetu kule Arusha amechinjwa na wabunge wetu
huko Mwanza wamekatwa katwa mapanga, tena mbele ya polisi….tuangalie
sana,”alitahadharisha Lissu katika mkutano huo wa hadhara.
Kuhusu
ushindi wa kesi iliyokuwa ikimkabili, ambayo ni moja ya mashauri 14
yaliyofunguliwa, kati ya majimbo 23 ya CHADEMA nchini, Lissu aliishukuru
mahakama kumuona hana hatia, ingawa anaamini wadai wa kesi hiyo wamepoteza fedha
nyingi, zinazofikia zaidi ya Sh. Milioni 200, ili ubunge wake
utenguliwe.
Aidha huo
ulikuwa mkutano wa kwanza kufanyika Singida mjini na watatu kimkoa,
tangu mahakama kuu, kanda ya Dodoma, kupitia Jaji Moses Mzuna wa Moshi,
Mkoani Kilimanjaro, kufutilia mbali shauri la kupinga ubunge,lililofunguliwa na wanachama wawili wa CCM.
No comments:
Post a Comment