Meneja
Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akikabidi msaada wa mabati
264 kwa sheha wa Stahabu-pemba bw haji Faki Komb ikiwa ni msaada wa
Airtel kushiriki kumalizia ujenzi wa kituo cha afya kwaajili ya
kuhudumia familia mbali mbali za maeneo ya STAHABU, CHOKOCHO, KIZUMGU,
KANDARANI na SHIDI. Katika hafla hiyo Airtel ilijitolea Bati 264,
Saruji 143, Nondo 62 pamoja na mbao vyote vyenye thamani ya 10/-tsh ili
kumalizia ujenzi wa kituo cha afya cha Michenzani pemba mwishoni mwa
wiki. Kati mwenye shati la drafti akishudia ni Afisa Mipango wa Wilaya
Mkoani Bw Omar Shehe Omari na anaefuata ni Sheha wa Michenzani Bw
Abdalah Omari.
Kampuni
ya simu za mkoni ya Airtel imeendeleza dhamira yake ya kushirikiana na
jamii sehemu mbali mbali kwa kuchangia ujenzi wa kituo cha afya
kilichopo kisiwani pemba maeneo ya michenzani kitakachosaidia kutoa
huduma maeneo ya STAHABU, CHOKOCHO, KIZUMGU, KANDARANI na SHIDI
Akiongea
wakati wa kukabidhi vifaa hivyo meneja wa Airtel Zanzibar Bw Hagai
Samson alisema “msaada huu wa Airtel kwa wakazi wa huku pemba hautaishia
hapa , leo tumejitolea Bati 264, Saruji 143, Nondo 62 pamoja na mbao
zitakazotumika kumalizia ujenzi wa kituo hiki cha afya tukiwa na imani
vikitumika kwa usahihi vitasaidia kuboresha huduma za afya katika maene
ya Michenzani, Chokocho, Kizumgu, Kandandarani na Shidi.
Airtel
Tanzania tunawashukuru sana wateja wetu mliopo pemba kwa kuwa ndio hasa
wanaotuunganisha na jamii hii siku ya leo. Tunachojitolea hapa ni
sehemu ya faida tunayoipata kila mnapozitumia huduma zetu zikiwepo
kupiga na kupokea simu, Airtel money pamoja na huduma yetu ya Internet
ya 3.75G.
Kwa
upande wake Sheha wa Michenzani akipokea msaada huo wa vifaa vya
ujenzi wa kituo hicho cha Afya aliishukuru Airtel na kuwaomba wadau
wengine wanaofanya biashara kisiwani huko kuiga mfano huo wa Airtel
“
naishukuru sana Airtel kwa msaada wao huu, utatusaidia sana kukamilisha
ujenzi wa kituo hiki cha Afya hapa michenzani, tunaamini hii ni
jitihada za kumuunga mkono Mheshimiwa raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Mh, Ally M. Shein ambae wiki moja iliopita aliweka
jiwe la msingi katika kituo hichi na kuhimiza ujenzi wa kituo hiki
uende kwa kasi ili kusaidia kupunguza adha ya mrundikano wa wagonywa
katika kituo kimoja kile cha Bogoa.
Nae
Afisa Mipango wa Wilaya ya Mkoani Omari Shehe Omari akiongea kwa niaba
ya Mkuu wa Wilaya hiyo alisema ujenzi wa kituo hicho cha Afya una lengo
la kupunguza matatizo ya afya yanayoikabili jamii inayoishi maeneo hayo
hasa kwa kuzingatia wakina mama na watoto.
“Ninaipongeza
Airtel sana kwa kujitolea na kutusaidia kufikia malengo yetu ya
Milenia, sisi tuna dhamira ya kuboresha Afya na elimu kwa pamoja, kila
Skuli iwe na kituo cha Afya au kila Shehia (Serikali ya Mtaa) iwe na
kituo chake cha Afya.
Hivyo kwa msaaada huu utasaidia sana serikali yetu kutifika malengo yake kwamba pia michenzani watapata kituo chao hapa karibu.”
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel ina mkakati wa kutoa misaada ya kijamii
kwa kugusa sekta za mazingira, Elimu na Afya kwa lengo la kuisaidia
serikali na jamii kwa ujumla kupambana na changamoto mbalimbali .
Mwaka
huu wa 2012 pia Airtel imejipanga kuhakikisha jamii iliyopo pembezoni
mwa nchi mbali na kupata huduma bora ya mawasiliano ikiwemo ile ya
Airtel money pia itashiriki kikamilifu katika miradi mbalimbali ili
kujenga vyema ushirikiano na jamii kama ilivyoshiriki kuboresha
miundombinu ya Afya Visiwani Zanzibar.
No comments:
Post a Comment