Pages

KAPIPI TV

Sunday, April 29, 2012

SIMBA YAICHAPA AL-AHLY SHANDY 3-0 UWANJA WA TAIFA DAR-ES-SALAAM

 Mchezaji wa timu ya Simba Mganda Emmanuel Okwi akikokota mpira kuelekea goli la timu ya Al Ahly Shandy, huku mchezaji wa timu ya Isaac Seun Malik wa timu ya Al- Shandy ya Sudan akijaribu kumzuia katika mchezo wa kombe la Shirikisho unaofanyika kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

  Mashabiki wa Simba wakishangilia uwanja wa Taifa jijini Dar-es-salaam


Timu ya Simba ya jijini Dar  imefanikiwa kuichabanga  Al Shandy ya Sudan magoli 3-0 katika kipindi cha lala salama na kutoka kifua mbele katika mchezo huo wa kwanza kabla ya ule wa Sudan wiki mbili zijazo.
 
Aidha katika mchezo huo wa vuta nikuvute magoli ya Simba yalifungwa na wachezaji Patrick Mafisango, Uhuru Selemani na Emmanuel Okwi, 
 
Hata hivyo mchezji Patrick Mafisango alikosa goli la penati baada ya mchezaji Emmanuel Okwi kuchezewa vibaya na beki wa timu ya Al Ahly Shandy katika kipindi cha kwanza.
 
Ushindi huo wa Simba umeibua hisia za mashabiki wake ambapo walitoka uwanjani kwa mbwembwe za aina yake.  

No comments: