N a,Mustapha Kapalata.
Igunga
BARAZA
la Madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Igunga Mkoani Tabora limelaani
vikali vitendo vinavyofanywa na baadhi ya wananchi kwa kuwatishia uhai
wa maisha wa tumishi wa Halmashauri hiyo.
Wakizungumuza
katika baraza hilo walisema kuwa watakao bainika na waliobainika kwa
kutishia uhai wa maisha ya watumishi na wafanyakazi wa mashirika
mbalimbali wachukuliwe hatua za kisheria.
Madiwani hao wameitupia lawama kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya kuwa taarifahizo inazo lakini utekelezaji ni wakusuasua.
Baraza hilo liliiagiza kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya kufuatilia haraka na sheria kali zichukuliwe mapema.
Walisema
kitendo cha kamati hiyo kukaa kimya kwa muda mrefu kwa kufanya
uchunguzi ni uzembe ambao mtu anaweza kuuawa bila sababu za msingi kwani
taarifa kama hizo zikifika zitolewe mapema katika vyombo vya dola ili
hatua zichukuliwe.
Kitendo
hicho cha kutishia maisha watumishi wasisimamie na kutekeleza miradi
kinarudiha nyuma m aendeleo ya jamii na kuongeza umasikini pamoja na
kuwatia hofu watumishi hao.
Katibu
wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilya Paul Mtenjela alisema kuwa
suala hilo linafanyiwa uchunguzi na kuongeza kuwa muda utakapo wadia
litafikishwa katika vyombo husika tayari kwa sheria kufuata mkondo wake
kwa watuhumiwa watakao bain ika.
Mkuu
wa Polis wilaya Issa Ismail Muguha alisema vitisho hivyo vya watumishi
havijafika ofisini kwake na kuongeza kuwa wote waliotishiwa maisha
wafike ofisini kwake tayari kwa kuchukua hatua za kisheria ikiwa
nipamoja na kufikishwa mahakamani kwa watakao bainika na tuhuma hizo za
kutishia uhai wa maisha ya watumishi na wananchi kwa ujumla.
Muguha
alisema endapo taarifa hizo zinge fika ofisini kwake hatua kari
zingechukuliwa kwa watuhumiwa hao tofauti na sasa watu hao bado wapo
uraiani haliambayo watumishi wanashindwa kufanya kazi zao vizuri.
No comments:
Post a Comment