Kichanga kilichotupwa kwenye Dampo Isevya sokoni |
Baadhi ya maafisa wa Polisi wakifanya kazi yao kufuatia kichanga hicho kilichotupwa kikiwa kimekufa |
Dampo lililotupiwa kitoto hicho kichanga |
Baadhi ya wafanyabiashara wa Soko la Isevya |
Maafisa wa Jeshi la Polisi wakijadili jambo katika tukio hilo |
Mtu asiyejulikana amekitupa kitoto kichanga kwenye dampo
lililopo kwenye Soko la kata ya Isevya manispaa ya Tabora
Kichanga hicho kinachokadiriwa kuwa na umri kati ya miezi
nane na tisa kimeokotwa na mtu mmoja anayedaiwa kuwa na magonjwa ya akili
ambaye alikwenda kutupa takataka katika dampo hilo na kukikuta kichanga hicho
kikiwa kimefunikwa na khanga.
Hata hivyo mtu huyo anayefahamika soko la Isevya kwa kazi ya
kubeba takataka,baada ya kugundua kichanga hicho kilichotapakaa damu nyingi
alikichukua na kukipeleka sokoni hapo huku akilalamikia kitendo cha kutupwa
kichanga hicho ambacho hakikuwa na uhai.
Baadhi ya wafanyabiashara wa soko la Isevya walistaajabu
tukio hilo huku zikiwashangaza zaidi kauli za mtu huyo ambaye huwa wakimfahamu
kwa mapungufu ya akili.
Kwaupande mwingine maafisa wa Jeshi la Polisi walifika eneo
la tukio na kuuchukua mwili wa kichanga hicho huku wakiwaomba wananchi kutoa
taarifa za mtu atakayebainika kuwa amehusika na tukio hilo la kinyama.
Hata hivyo katika kata ya Isevya matukio utoaji mimba na kutupa watoto yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara ingawa mara nyingi wanaojihusisha na matendo hayo wamekuwa wakifichwa
No comments:
Post a Comment