Pages

KAPIPI TV

Friday, April 27, 2012

MWENGE WA UHURU KUHAMASISHA SENSA YA WATU NA MAKAZI NCHINI

Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Vijana Dk. Kissui Steven akiongea na waandishi wa habari kuhusu sherehe za kuwashwa kwa  mwenge wa Uhuru zitakazofanyika mkoani Mbeya tarehe 11 Mwezi wa tano . Moja ya kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru ni kuwahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi la sensa ya watu na makazi  litakalofanyika nchini kote kuanzia tarehe 26 Augosti mwaka huu. Kulia ni Afisa Uhamasishaji sensa ya watu na Makazi Said Amir.
Picha na Anna Nkinda - Maelezo
Mratibu wa Sensa ya watu na makazi  kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Irenius Ruyobya akiongea na waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa wananchi kujibu kwa ufasaha maswali watakayoulizwa wakati wa zoezi la sensa ya watu na makazi  litakalofanyika kote nchini kuanzia tarehe 26 Augosti mwaka huu. Jumla ya shilingi bilioni 141 zitatumika hadi kukamilika kwa zoezi hilo.
Afisa Uhamasishaji sensa ya watu na Makazi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Said Amir akiwashukuru waandishi wa habari kutokana na jitihada zao za kuwaelimisha  wananchi kuhusiana na zoezi la sensa ya watu na makazi  litakalofanyika nchini kote kuanzia tarehe 26 Augosti mwaka huu. Hii ni Sensa ya tano kufanyika hapa nchini tangu kupatikana kwa uhuru mwaka 1961.
Afisa Uhamasishaji sensa ya watu na Makazi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Said Amir akiwaonyesha waandishi wa habari vitabu vyenye maelezo mbalimbali kuhusiana na sensa ya watu na makazi itakayofanyika kote nchini kuanzia tarehe 26 Augosti mwaka huu. Jumla ya shilingi bilioni 141 zitatumika hadi kukamilika kwa zoezi hilo pia hiyo ni Sensa ya tano kufanyika tangu kupatikana kwa uhuru mwaka 1961.

No comments: