Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na Mkuu wa Jeshi la akiba
nchini Brigedia Generali R.M Muhuza hayupo pichani katika ofisi yake leo
alipomtembelea kujitambulisha na kueleza juu ya ujio wake Mkoani Rukwa ambapo ni
kuona matayarisho ya kikosi cha mgambo cha Mkoa wa Rukwa ambacho kitashiriki
kwenye zoezi la kijeshi litakalohusisha Vikosi vya JWTZ vilivyopo katika Mikoa
ya Nyanda za Juu Kusini (Ruvuma, Mbeya, Rukwa, Iringa, Lindi, Mtwara, Njombe na
Katavi) ifikapo tarehe 15 Septemba 2012. Zoezi hilo la kijeshi litaandaliwa na
Brigedi ya 401 KV iliyopo Songea Mkoani Ruvuma. Jumla ya Wanamgambo 60 kutoka
Mkoa wa Rukwa wanatarajiwa kushiki zoezi hilo litakalojumuisha vikundi toka
Kamandi zingine za Ndege za Kivita, Wahandisi, Mizinga na Vifaru. (Picha na
Hamza Temba- Ofisi ya Mkuu wa Mkoa RUKWA"rukwareview.blogspot.com " )
Kutoka
kushoto ni Mkuu wa Jeshi la akiba nchini Brigedia Generali R.M Muhuza,
Msaidizi wake Kanali A.Y Amasi na Katibu wake Meja A.R Gumbo kutoka Makao Makuu
ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania Dar es Salaam wakizungumza na Mkuu wa Mkoa wa
Rukwa walipomtembelea Ofisini kwake leo. (Picha na Hamza Temba- Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa RUKWA"rukwareview.blogspot.com " )
Mazungumzo
yakiendelea. (Picha na Hamza Temba- Ofisi ya Mkuu wa Mkoa RUKWA"rukwareview.blogspot.com " )
Miongoni
mwa mambo aliyosisitiza Mkuu huyo wa Mkoa ni uboreshwaji wa sekta muhimu nchini
kama sekta ya ulinzi ili kuepusha uvunjifu wa amani iliyodumu nchini kwa muda
mrefu. Alisema Jeshi la Wananchi lina jukumu kubwa la kuhakikisha amani
inakuwepo nchini na sio kutokana na hatari zinazoweza kutoka nje bali kwa hatari
zinazoweza kusababishwa na wananchi wenyewe. (Picha na Hamza Temba- Ofisi ya
Mkuu wa Mkoa RUKWA"rukwareview.blogspot.com " )
No comments:
Post a Comment