Pages

KAPIPI TV

Wednesday, April 11, 2012

NINI HATMA YA SOKA LA TABORA NA SEKTA YA MICHEZO KWA UJUMLA?


Na Hastin Liumba,Tabora

SOTE tunatambua kuwa michezo duniani ni afya,furaha na ajira na hakuna
ubishi michezo yoyote duniani kwa sasa inalipa na ni ajira kubwa
linaloingiza fedha ngazi ya mtu mmoja mmoja,familia na taifa kwa
ujumla.

Hebu leo nizungumzie,kwa kifupi, mchezo wa soka kwa sasa duniani
umeweza kutoa ajira kwa wachezaji wa mchezo huo na umekuwa lulu kwa
mashabiki hasa pale inapofikia mwishoni mwa mashabiki hasa wengine
hutazama katika runinga hadi nyakati za usiku wa manane.

Hii yote ni kuonyesha mchezo wa soka licha kuwa na mashabiki lukuki
bado ni mchezo bila ya kumung`unya maneno unaingiza fedha nyingi
katika ngazi ya vilabu,wachezaji wenyewe,na mataifa husika.

Napenda sasa nizungumzie mchezo wa soka hapa Tabora,nalazimika kutamka
kuwa kila kukicha mchezo huo unazidi kupotea,katika ramani yake,kwani
licha ya kutopewa kipaumbela na uongozi wa chama mpira wa miguu mkoa wa Tabora(TAREFA).

Aidha wakati hali ya mchezo wa soka inakuwa ni hadithi ya abunuasi,kurejea kwenye ramani yake kama ilivyokuwa enzi ya timu Mirambo miaka ya 1994 hadi kipindi cha mwaka 2000.

Kidogo labda nizungumzie hali ya chama cha soka Tabora(TAREFA), kwa ufupi kwani sina lengo la kuuzungumzia uongozi,Chama hiki kiko kaburini kwa sasa kwani hata mipango ya
kuendesha soka kwa uongozi wake umebaki mazoea tu.

Chini ya uongozi wa mwenyekiti wa TAREFA,Ismail Aden Rage na katibu
wake,Albart Sitta,viongozi hawa walishindwa kabisa kuinua soka la mkoa wa Tabora na kuishia kurumbana kutwa-kucha na kusababisha  baadhi ya wajumbe kadhaa wa kamati ya utendaji kuachia ngazi akiwemo Rage mwenyee kwa kigezo cha chama kugubikwa na migogoro ingawa baadae Rage akajizunguuka mwenyewe na kuikana kauli yake kana kwamba ni mchezo wa kuigiza ua komedi ya mitaa ya uswahilini.

Wakati hayo yakiendelea kuwepo leo soka ya mkoa wa Tabora kamwe haitaweza kufikia malengo endapo hakuna mipango mizuri ya viongozi,hakuna maeneo ya watoto kushiriki michezo.

Licha maeneo mengi ya wazi kuuzwa,hata kile kiwanja cha Ali Hassan Mwinyi kiko hoi kwani chama cha mapinduzi,(CCM),mkoa wa Tabora kimeshindwa kuuhudumia uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 34,000 wakiwa wameketi.

Uwanja huo kwa sasa umegubikwa na nyasi,kama haitoshi basi uwanja huo baadhi ya maeneo yamejaa maji kiasi cha samaki aina ya Kambare pengine wameanza kuzaliana.

Hakuna ubishi CCM wameshindwa kuhudumia uwanja huo,kwani hata mashindano ya Kilimanjaro taifa Cup yanapoanza,uwanja huo nyasi zake hufyekwa haraka haraka kwani unakuwa umesahaulika muda mrefu
kuhudumiwa.

Hali hiyo ya uwanja kuzungukwa na maji, inanilazimu kuutafuta uongozi wa chama cha mapinduzi,(CCM),mkoa wa Tabora ili kuweza kupata maelezo ni jinsi gani maeneo ya michezo hususani uwanja wa Ali Hassan Mwinyi umefikia hatua hiyo mbaya ambayo haifai hata kuzungumziwa mbele ya hadhara.

Katibu msaidizi mkuu na mhasibu wa CCM mkoa wa Tabora,Charles Sangula anaeleza na kukiri kuwa ni kweli hali ya uwanja wa Ali Hassan Mwinyi ni mbaya lakini licha CCM kuwa ni mmiliki bado uwanja huo una kiongozi anayeusimamia.

Sangula anasema kuwa pamoja na hali hiyo wamekuwa wakiufanyia matengenezo kadhaa ikiwemo ufyekaji nyasi zake pale inapohitajika.

Hata hivyo katibu huyo anausukumia mpira wa maelezo kwa meneja wa uwanja huo,Hamis Murad kuwa anapaswa kuulizwa zaidi kwani uongozi umempa majukumu ya usimamizi wote lakini usimamizi wa huyo Meneja Muradi hauna mashiko hata kidogo kwani hana kauli wala uwezo wa kuchukua fungu la fedha zinazopatikana  katika uwanja huo na kuzitumia kwa ajili ya kuusafisha.

”Nafikiri ukitaka majibu mazuri zaidi ni kwani nini uwanja unafikia hatua ya kuwa katika sura ya hali ile wakati uwanja una kiongozi wake msimamizi.......na zaidi baada ya hali ya nyasi kuota na kurefuka
zaidi mimi niliamua kuomba walimu wanipatie wanafunzi na wamefyeka
umekuwa safi.” Alisema Sangula wakati haoni kuwa kufanya hivyo ni kinyume kwakuwa fedha za uwanja huo zinafanyakazi gani au zinakwenda wapi.

Naamua kumtafuta meneja wa uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Hamis Murad naye bila kumung`unya maneno anasema hali ya uwanja atafutwe katibu msaidizi wa CCM mkoa wa Tabora,Charles Sangula ndiye atajibia kwa usahihi,sasa unaona ni jinsi gani hawa CCM wanavyoshindwa kuuhudumia uwanja huo ambao kwa sasa tuseme unazeeka baada ya kukomaa kwa muda mrefu.

Murad anaeleza kuwa hali ya uwanja ni kweli mbaya na hata yale maji yaliyopo mbele ya uwanja huo yanatia kinyaa lakini hana jinsi kwani anashindwa kuwajibika ipasavyo na kipo kinachomkwamisha,(hakukitaja).

Bila ya kusema ni kitu gani kinamkwaza ashindwe kuuhudumia uwanja huo Murad anakwepa na kudai hana majibu yoyote na utafutwe uongozi wa juu wa CCM mkoa wa Tabora.

”Nitamke tu kuwa mtafute katibu msaidizi na mhasibu,Sangula......atakupa majibu sahihi ni kwanini uwanja unakuwa hivyo mimi kuwa meneja siyo kigezo yapo mambo yananikwaza au siyo.”
Alisema Murad.

No comments: