Msichana Elizabeth ' Lulu' Michael ameyasema hayo Mahakamani Kisutu hii leo. Kauli hii inapingana na taarifa kuwa ana miaka 18.
Muigizaji huyo maarufu nchini anayehusishwa na mauaji ya mwigijazi mwenzake Steven Kanumba amepandishwa leo kizimbani kwenye mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar-es-salaam na kusomewa mashtaka yake ambayo yanamhusisha na mauaji hayo yaliyotokea April 7 mwaka huu.
Elizabeth Michael "LULU"amesomewa mashtaka hayo mbele ya hakimu mkazi Augustino Mmbando na wakili Elizabeth Kaganda ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi April 23 mwaka huu.
Hata hivyo LULU aliletwa mahakamani hapo mapema asubuhi kwa usafiri wa gari aina ya Suzuki Grand Vitara lenye nambari za usajiri T 848 BNV,gari ambalo liliingia kwa kasi kiasi cha kuwafanya baadhi ya waandishi wa habari waliokuwapo mahakamani hapo kukosa fursa ya kumpiga picha msanii huyo ambaye kwasasa anakabiliwa na tuhuma ya kesi ya mauaji.
No comments:
Post a Comment