Pages

KAPIPI TV

Thursday, April 12, 2012

MTOTO ADUMBUKIA KWENYE PIPA LA POMBE YA MOTO"Wazazi wamkimbiza hospitali pasipo kutoa taarifa Polisi,hali yake kwasasa mashakani"


 MTOTO mdogo mwenye umri wa miezi miwili na nusu kama sijakosea kwa mujibu wa maelezo ya mama yake mzazi Bi.Mosi Ramadhani(26)amedumbukia kwenye pipa la pombe  ya kienyeji iliyokuwa ikipikwa  aina ya KOMONI katika kijiji cha Kalumwa eneo la manispaa ya Tabora.

Mtoto huyo ambaye anaitwa Malongo Kassim inadaiwa wakati wakicheza na wenzake huku akiwa amebebwa mgongoni na mtoto mwenzake aliyefahamika kwa jina la Holo Kulwa mwenye umri wa miaka sita,alichomoka kutoka mgongoni na kuangukia kwenye kipande cha pipa lililokuwa likichemshiwa pombe hiyo.

Maelezo ya mama mzazi wa mtoto huyo Bi.Mosi,mara baada ya mtoto huyo kuopolewa na mwenzake aliyekuwa amembeba mgongoni tayari alikuwa amekwisha ungua maeneo mbalimbali ya mwili wake kutokana na uji mzito wa unga wa mahindi yaliyochanganywa na mtama ambao ulikuwa umechemka  na hata kusababisha mtoto huyo aliyemuopoa naye akaungua begani na sehemu ya tumbo lake.

"Mimi nilikuwa napasua kuni kwa ajili ya kupika chakula cha jioni,ghafla nilimuona mtoto wangu akiwa amebebwa na mwenzake huku wakilia kwa sauti ya juu,na nilipomuangalia tayari walikuwa wameungua sana wote wawili."alisema Bi.Mosi wakati akiongea na mtandao huu katika hospitali ya mkoa wa Tabora Kitete ambako kwasasa amelazwa akipatiwa matibabu.

Hata hivyo pamoja na kupatiwa maelezo ya nini kilichowasibu watoto hao wawili ambao mkasa huo walikumbana nao kwenye nyumba ya jirani ambako pombe hiyo inapikwa licha ya kuwa si eneo rasmi la kilabu cha pombe hiyo ya kinyeji,Bi.Mosi akiwa na mumewe walimkibiza mtoto huyo Malongo Kassim hadi hospitali ya mkoa wa Tabora Kitete.

"Kwakweli sisi hatujapitia Polisi kutoa maelezo ya mkasa huu ingawa hali ya mtoto huyu kwasasa inaendelea kuwa mbaya kiasi hiki"alisema baba mzazi wa mtoto huyo Bw.Kassim Masoud ambaye alidai kuwa tukio hilo lilitokea kwa jirani yao aitwaye Mwanamaganga ambaye ni maarufu kijijini kwao hapo Kalumwa kwa upikaji wa Pombe za kienyeji ikiwemo aina ya Gongo.

Hata hivyo hali ya mtoto huyo Malongo Kassimu si nzuri kwa mujibu wa maelezo ya wauguzi wa wadi namba kumi na moja ambayo watoto hulazwa.

        



No comments: