Ndugu zangu,
Ni
kazi ngumu kuwa wakili kwa anayeonekana na jamii kuwa ni ‘ shetani’.
Lakini, kwenye hili la kifo cha kusikitisha cha msanii Steven Kanumba
kuna haja ya kukaa chini na kutafakari kwa bidii.
Kuna maswali pia ya kujiuliza juu ya msichana huyu wa miaka 18 ambaye sehemu kubwa ya jamii imeshamuhukumu kuwa ni muuaji.
Kuna hata ambao hawalijui jina lake la kamili, bali, anajulikana kama ‘ Lulu’. Jina lake ni Elizabeth Michael .
Simulizi
ya Lulu inaonyesha kuwa yeye na Kanumba walikuwa na mahusiano. Na wivu
pia umeingia kwenye mahusiano yao. Hivyo basi, ugomvi na hatimaye kifo
cha Kanumba.
Uchunguzi
kamili haujakamilika. Na kama haujakamilika, basi, Lulu anabaki kuwa ni
mtuhumiwa na si muhusika na kifo hicho. Kumwita Lulu muuaji ni
kuharakisha kutoa hukumu isiyo ya haki.
Pamoja na machungu yetu, lakini
wanadamu tunapaswa kuwa na subira.
Na
ukweli unabaki, kuwa Lulu ni mwanadamu kama wewe na mimi. Na kwa yote
yaliyotokea, anabaki kuwa ameondokewa na mpenzi wake. Je, ni nani
anayemfariji msichana huyu wa miaka 18 aliyeondokewa na mpenzi wake?
Na. Mdau Maggid Mjengwa
"TUKUMBUKE LILILOMPATA LULU LINAWEZA KUMPATA MTU YEYOTE YULE ILI MRADI BADO UKO HAI NA PIA UKO NA KUSHIRIKIANA NA BINADAM WENZAKO KATIKA MASUALA MBALIMBALI YA KIJAMII''.
Na.Juma Kapipi.
No comments:
Post a Comment