Mmoja wa wasafiri walionusurika katika ajali ya ndege hiyo leo iliyotokea leo hii asubuhi huko Kigoma |
Abiria wapato 35 na wafanyakazi wanne wa ndege ya Shirika la ndege nchini ATC wamenusurika katika ajali ya ndege iliyotokea leo hii asubuhi katika uwanja wa ndege wa Kigoma majira ya saa 4:15.
Taarifa ya awali zilizotufikia zinaeleza kuwa ndege hiyo aina ya Dash 8-300 iliyokuwa inatoka Kigoma kupitia Tabora kwenda Dar-es-Salaam ilipata ajali baada ya kuteleza na kuangukia ubavu wa kulia katika tope jingi lililopo njia ya kurukia uwanjani hapo.
Kwa mujibu wa taarifa hizo,abiria na wafanyakazi wote waliokuwa wakisafiri katika ndege hiyo walifanikiwa kutoka salama baada ya jaribio la kutaka kupaa kushindikana katika uwanja huo.
Baadhi ya abiria walionusurika wamewasifia marubani wa ndege hiyo Bw.Emmanuel Mshana na msaidizi wake Bw.Mbwali Masesa kwa jitihada zao katika kuidhibiti ndege hiyo na kuokoa maisha ya watu waliokuwamo katika usafiri huo.
Uchunguzi wa awali umeonesha kuwa bawa la kulia pamoja na injini ya propel ya upande huo vimeharibika vibaya.
No comments:
Post a Comment