Pages

KAPIPI TV

Monday, April 9, 2012

JESHI LA POLISI LATOA TAARIFA ZA AWALI KUHUSU KIFO CHA KANUMBA

RPC wa Kinondoni-Charles Kenyela

Pombe kali (Whisky) aina ya Jacky Daniel, imetajwa kama chanzo cha kifo cha mwigizaji nyota wa filamu nchini, Steven Charles Kanumba aliyefariki usiku wa kuamkia jana nyumbani kwake, Sinza, Dar es Salaam.

Kamanda wa Polisi Kinondoni, ACP Charles Kenyela amesema leo kwamba uchunguzi wa awali unaonyesha hivyo, lakini bado wanaendelea na uchunguzi zaidi, ili kujua taarifa sahii kuhusu kifo hicho.

ACP Kenyela amesema kwamba  wamefanikiwa kumuhoji mtuhumiwa wa kwanza katika tukio hilo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na katika maelelezo yake amekanusha kumsukuma Kanumba.

Vyombo vingi vya habari vilimnukuu ndugu wa Kanumba, Sethi jana akisema kwamba Lulu alimsukuma mwigizaji mwenzake huyo katika ugomvi wao wa wivu wa kimapenzi hadi akaanguka na kufariki dunia.

Akizungumza kutokana na maelezo ya Lulu, Kamanda huyo alisema kwamba; ugomvi wao ulitokana na Kanumba kutaka kumdhibiti Lulu wakati akizungumza na simu.

“Kanumba aliamua kumfuata Lulu nje huku akifoka kwa sauti, akitaka aelezwe kwa nini alitoka nje kupokea simu, huku akimtuhumu kuwa huenda alikuwa akizungumza na mwanaume mwingine.

Baada ya Lulu kuona Kanumba anamfuata, aliamua kukimbia kutoka nje ya geti, lakini kabla hajafanikiwa kufungua geti, Kanumba  alimkamata na kumrudisha ndani. Kanumba akiwa amemshikilia, waliingia wote chumbani na kufunga mlango. Sasa haijulikani nani aliyefunga mlango, ingawa maelezo ya Lulu, anadai kuwa aliyefunga mlango ni Kanumba,”alisema Kamanda huyo.

Akiendelea kumnukuu Lulu, Kamanda Kenyela anasema; “Baada ya Kanumba kufunga mlango, alimuona akilegea na kujigonga kisogo chake kwenye ukuta wa chumba hicho kabla ya kuanguka chini,”alisema.

Alisema uchunguzi wa tukio zima ukikamilika, hatua inayofuata ni kumpeleka Lulu mahakamani kama mtuhumiwa wa mauaji.

Aidha Jeshi la Polisi lilichukua kama ushahidi, pombe hiyo whisky aina ya Jacky Daniel,soda aina ya Sprite pamoja na panga ambavyo inadaiwa vilikutwa eneo la tukio ingawa vitu hivyo havijahusishwa moja kwa moja katika tukio hilo.

Hata hivyo kamanda Kenyela aliongeza kwa kusema kuwa uchunguzi wa madaktari ndio utakothibitisha ukweli wa kifo cha nguli huyo wa filam nchini Steven Kanumba,na kwamba taarifa za uchunguzi wa madaktari zitapelekwa mahakamani na si za kutolewa kiholela.

Kwaupande mwingine Kamanda Kenyela alisema barabara ya Kinondoni italazimika kufungwa kufuatia shughuli za mazishi ya msanii huyo ambazo zinadaiwa kufanyika hapo kesho.

No comments: