Bi.MARIAM WILMORE:Mjumbe wa Bodi ya Bima ya Afya NHIF,kimsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Madereva wa Bodaboda mjini Tabora wakati akitoa shukrani kwa msaada wa Sare walizopewa na NHIF. |
Bw.EMMANUEL HUMBA:Mkurugenzi mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wakati akizungumza na waendesha Bodaboda mjini Tabora. |
Bw.SALUMU MBOGA:Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora kitengo cha usalama barabarani |
Uongozi ngazi ya juu wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF
umewataka waendesha bodaboda kujiunga na mfuko wa afya kwa jamii CHF ili uwe na
msaada kwao na hasa wakati wa kuhitaji huduma ya matibabu.
Mkurugunzi mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya nchini
Bw.Emmanuel Humba akizungumza katika zoezi la ugawaji wa sare za usalama kwa
waendesha Bodaboda mjini Tabora alitumia fursa hiyo pia kuwataka kuwa makini
wakati wanapotumia vyombo hivyo vya usafiri wa pikipiki ili kuepuka ajali
zisizo za lazima.
Mbali na tahadhari hiyo ambayo pia ililenga kuwakumbusha
ajali nyingi zinazojitokeza ambazo husababishwa na waendesha vyombo hivyo vya
usafiri pia aliwataka wajiunge na mfuko wa Afya kwa jamii CHF ambao alieleza
kuwa utawasaidia na hasa wakati wanapokumbwa na majanga ya ajali barabarani
yatakayowalazimu kuhitaji matibabu.
Kwaupande wake mjumbe wa bodi ya NHIF Bi.Mariam Wilmore
akizungumza na waendesha Bodaboda hao kabla ya kugawa sare hizo aliwataka
madereva hao kuiheshimu kazi yao na kuona kuwa ni kazi kama kazi nyingine
halali ambayo inaweza kuwasidia kuendesha maisha yao ya kawaida.
Akizungumzia suala la usalama kwa waendesha Bodaboda hao
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora kitengo cha Usalama barabarani Bw.Salumu Mboga
aliipongeza Bima ya Afya kwa hatua ya kuwafikiria madereva hao wa Bodaboda kwa
kuwapatia sare hizo na huku akiwataka waanze kuzivaa kutokana na ukweli kwamba
zina rangi maalum inayowezesha kuonekana kwa urahisi hasa nyakati za usiku wawapo
barabarani na hivyo kupunguza uwezekano wa ajali zisizo za lazima.
No comments:
Post a Comment