Pages

KAPIPI TV

Monday, April 2, 2012

AJIRA KWA WATOTO KATIKA MASHAMBA YA TUMBAKU YAZIDI KUSHAMIRI TABORA"Inazidi kuathiri kiwango cha elimu kwa wanafunzi"


Ingawa ni jambo ambalo linaonekana kana kwamba ni kitu cha kawaida kwa baadhi ya jamii ya wakulima katika vijiji mbalimbali mkoani Tabora lakini ni ukweli usiopingika ongezeko la vitendo vya utumikishwaji kwa watoto katika mashamba ya tumbaku umekuwa ukishamiri na kuathiri hata viwango vya elimu kwa wanafunzi.

Pengine nikisema baadhi ya watoto wanapelekwa shuleni na wazazi wao kwa lengo la kutaka kukua au kusaidia malezi ya kawaida pekee, naweza nisieleweke waziwazi lakini ushahidi juu ya hilo kuna idadi kubwa ya wanafunzi kuanzia darasa la kwanza hadi la saba hawajui kuandika wala kusoma.

Wengi wao hata kwenda shule imejidhihirisha kuwa ni wakati ule tu mtoto au mwanafunzi anapokuwa hana kazi za lazima za nyumbani  ndio inaonekana kuwa kuna umuhimu wa kuhimizwa kwenda shule.

Kwa Taifa gani ambalo linaandaliwa kwa watoto walioko vijijini?...

Wilaya zote za mkoa wa Tabora zinazojihusisha na kilimo cha tumbaku hakuna wilaya hata moja ambayo sijaona mtoto hatumiki kwenye shamba la tumbaku.

Iwe ni shamba la nyumbani kwao au la kufanya kibarua ili mradi ajipatie pesa kidogo kwa ajili ya kununua hata kivazi tu.

Kuanzia msimu wa kuandaa shamba,viatalu hadi msimu wa mavuno ya tumbaku,mtoto au mwanafunzi ni kuingia shughulini tu hadi wakati wa kungojea malipo ya mauzo ya zao hilo.

Wakati mwingine walimu wanaofundisha shule za vijijini wanakosa la kusema kuhusu ongezeko la watoto wasiojua kusoma na kuandika kwani tayari wanakuwa wamekwisha piga kelele kwa wazazi kuwapatia muda watoto wao wa kuhudhuria mafunzo darasani  lakini hakuna mafanikio.

Walimu wanalazimika kufunga kauli zao na kuangalia maslahi yao katika kutekeleza wajibu wao haijalishi watoto wanaelimika au la hilo sio jukumu lao. 

0767 456 259 au 0784 456 259 au 0655 456 259
jumakapipi@yahoo.com      

No comments: