Pages

KAPIPI TV

Saturday, March 31, 2012

WANAUME WAKIMBIA FAMILIA ZAO IGUNGA WAKIHOFIA KUUAWA"Ni kutokana na mgogoro wa ardhi unaohusisha familia mbili"

Mama mwenye mtoto mchanga wa siku 17,Mbalu Madakila ambaye alisema alivamiwa na kundi hilo usiku wa saa tisa,ambalo lilikuwa likimtaka awaoneshe baba yake,Madakila Cheyo ili wamuue,Mama huyo alisema alitundikwa juu ya mti wakitaka kumuua lakini walishauriana na kumuacha huru.
Baadhi ya nguo za famila zilizokimbia makazi yao zikiwa juu ya mti baada ya kundi linalojiita A-Shabab kuvamia kwa lengo la kuua.

Na Hastine Liumba
Igunga.
UONGOZI wa serikali ya kijiji cha Jogohya,wilaya ya Igunga,mkoani
Tabora,umesema uko mbioni kuachia ngazi baada ya serikali ya wilaya
kuwapuuza katika kumaliza mgogoro wa ardhi  kijijini humo.

Wakizungumza na mwandishi wetu kijijini hapo,wakiongozwa na metndaji wa
kijiji hicho,Yohana Ngehu,walisema wanashangazwa na hatua ya serikali
ya wilaya kushindwa kutatua tatizo lililopo na kupelekea baadhi ya familia
kuzikimbia nyumba zao kutokana na mgogoro wa ardhi uliopo.

Ngehu alisema mgogoro uliopo unasababishwa na Lutoba Masaka,na mtoto
wake Mathias Lutoba ambaye ameunda kundi linalojiita AL-SHABAB kundi linatafuta
familia zilizokimbia ili wafanye mauaji wakilazimisha kupora ardhi ya
Kija Tungu ambaye amekimbilia mjini Tabora kuhofia kuuawa.

Ngehu ameeleza kuwa pamoja kamati ya ulinzi na usalama kufika kijijini
hapo mwezi januari 10,mwaka 2012 na kujionea hali halisi ya mgogoro
hadi kupelekea kifo cha mwananchi mmoja aliyefahamika kwa jina la Mbalu Gigunwa ,bado wameendelea kukaa kimya hadi familia hizo zikaamua kwenda mafichoni.

"Tunamuomba mkuu wa mkoa Fatma Mwassa aingilie kati kwani mkuu wa
wilaya Fatma Kimario ameshindwa kumaliza mgogogro huo pamoja na kamati
yake ya ulinzi na usalama." alisema.

Ngehu anasema kijiji chake kina vitongoji sita ambavyo ni Bugembe
inayoongozwa na mwenyekiti wake Solo Lumala,kitongoji cha Mwaholi
kinaongozwa na Lugandya Lugandu,Kitongozi cha Mwamapela kinaongozwa na
Yohana Mabula.

Alitaja vitongoji vingine kuwa ni Mwamabeshi kinaongozwa na Silvester
Maige,Mwabali kinaongozwa na James Singu,Jogohya kitongoji
kinachoongozwa na Mwanamila Igunguli wote ni kupitia CCM.

Alisema wameshakutana na kukubaliana kuachia ngazi ili kijiji hicho
kiwe hakina uongozi kwani kama walinzi wa amani halafu wanapuuzwa na
uongozi wa wilaya huku hofu ikiwa imetanda miongoni mwao.

Kwaupande wao  wazee wa kijiji hicho walilieleza  kuwa wamechoshwa na
kituo cha polisi Igunga kwa kumlinda Mathias Lutoba ambaye wanaamini
ndiye wa kushikwa kwani ameshafanya uharibifu mkubwa kijijini hapo na
kusababisha baadhi ya wanaume kukimbia familia zao.

Wazee hao walisema kundi linaoongozwa na Mathias Lutoba,ambalo
linajiita AL-SHABAB,na kutangaza kufanya mauaji huku ripoti za familia
zinazowindwa zikiwa zimeshatoa taarifa kituo cha Polisi Igunga.

Kundi hilo la AL-SHABAB linaundwa na James Fale, Shengu Thomas,Shinge Lutoba,Kulwa Thomas na Luyombila Chenge huku wengine wawili wakiwa hawajulikani ambapo kundi hilo limeshapiga
watu wengi baada ya kukuta nyumba kadhaa hazina wanaume wanaodaiwa kukimbia.

Wazee hao walisema chanzo cha mgogoro huo ni Lutoba Masaka kuazimwa
ardhi ya kulima hekari 22 kati ya hekari zaidi ya 200 mali ya Kija
Tungu,lakini alipotaka kudhulumu ndipo mgogoro ulipoanzia.

Wameongeza kuwa kamati ya ulinzi na usalama ilipokuja kijijini hapo iliitisha
mkutano wa hadhara na kuuliza wananchi juu ya ardhi kuwa nani mmiliki
ndipo kura zote ziliposema ardhi hiyo ni mali ya Kija Tungu na Lutoba
Masaka hana ardhi lakini serikali imeshindwa kumaliza mgogoro huo.

"Tumechoshwa na Mathias Lutoba na baba yake kufanya kijiji
kisitaawalike nasi tunaweza kumuua siku atakapokanyaga kijijini
hapa.....maana polisi wanamlinda na yeye anatamka polisi wako mfukoni
mwake." walisema.

Wameeleza kuwa hadi sasa kuna familia yenye watoto watano wazazi wao
wametoweka hawajulikani walipo na mwananchi Thomas Tuli anatunza watoto hao hadi sasa hawaendi shule kwani mali zao zimeharibiwa vibaya
huku daftari zikichomwa moto.

Aidha wazee hao walisema kuwa hata mama mmoja ambaye ni Mwanankinda
ambaye alichukuliwa na kundi hilo nyumbani kwake usiku wa saa tisa
wakimtaka awapeleke kijiji cha Imalanguzu kijiji  ambacho kundi
hilo lilidai mume wa mama huyo,Mathalu amejificha hajulikani alipo.

"Yule mama alichukuliwa majira ya saa tisa usiku na kundi hilo hadi
sasa hajarejea nyumbani kwake tunahofia huenda kauawa na polisi wana
taarifa hizi bado wako kimya.walisema wazee hao.



No comments: