Pages

KAPIPI TV

Friday, March 30, 2012

MTOTO AFANYIWA UKATILI NA MAMA WA KAMBO",Aliwekewa Pilipili kwenye Macho,kuna hatari ya kuwa kipofu"

 Ukatili uliofanywa na mama wa kambo dhdi ya mtoto huyo huenda ukasababisha akawa kipofu


 .
 Na Anthony Mayunga –Mara
 Machi 30,2012.
 DAWATI la jinsia na Watoto la Jeshi la Polisi mkoa wa Mara limemwokoa
 mtoto  Samweli  Mussa Nyamatimbo(10)mkazi wa Nyakato NHC- Mwanza
 ambaye yuko kwenye hatari  ya kupofuka macho yake kutokana na vitendo
 vya ukatili aliokuwa akifanyiwa  na mama yake wa kambo wa kumwekea
 pilipili kwenye macho kwa muda mrefu hali ambayo imepelekea mtoto huyo
kutoona vizuri kwasasa.

Kwa mjibu wa maelezo ya mtoto huyo alidai kuwa alilazimika  kutoroka
 nyumbani kwao baada ya mateso kuzidi na kukimbilia Musoma kumtafuta
 baba yao ambaye alidai kuwa amewatelekeza kwa muda mrefu.

Akisimulia mkasa huo kwa kusita sita alisema kuwa mama yao wa kambo
anaye julikana kwa jina  maarufu  la Mama Leso leso  alikuwa akiwatesa yeye na mdogo wake wa kike  kwa kuwawekea pilipili kwenye macho kwa madai kuwa hawezi kulea watoto wasiokuwa wake.

Na kuwa mateso hayo yamedumu kwa muda mrefu na baba yao akawa
haonekani nyumbani ,na hata walipokuwa wakifanikiwa kumpata stendi ya
mabasi Buzuruga hakuonyesha kujali na hata kufika nyumbani kuwaona.

 Na kuwa licha ya juhudi za kumwona baba yao ambaye alidai ni kondakta
 kwenye kampuni ya Zakaria Express hazikuzaa matunda,”kila tukimfuata
stendi na kumweleza alikuwa hajali kabisa na amekuwa mbali na sisi baada ya kumfukuza mama".
 
Alivyosafiri.
Alisema kuwa katikati ya mwezi huu alilazimika kutoroka nyumbani kwao na kupanda Hiace mpaka Magu na kutelemka ,lakini hakupata msaada na kisha akapanda basi la Batco hadi Musoma na baada ya kuonekana hana uelekeo wahusika wa gari walimkabidhi kwa polisi wa kituo cha stendi Bweri ambao walijulisha dawati la  jinsia na watoto la jeshi la polisi.

Na kuwa lengo lake ni kumtafuta baba yao na kuepuka mateso aliyokuwa anapata ,huku akikiri kuwa kuondoka kwa mama yao kumewapa pigo kubwa yeye na mdogo wake kwa kuwa hata kusoma ameacha akiwa darasa la pili .

 Alidai kuwa mama yao alikuwa akipigwa na kuteswa na baba yao mara kwa mara na kulazimika kuondoka na kuoa huyo mama yao wa kambo.

Katibu wa dawati la Jinsia na Watoto la Jeshi la Polisi mkoa wa Mara Sajenti Johari Ngoma amemueleza mwandishi wetu  kuwa juhudi za kumpata baba yao hazijazaa matunda baada ya kuwasiliana na ajenti wa mabasi ya Zakaria Express na kudai kuwa hawana mtu mwenye jina hilo.

 “Huenda wameficha ama hayupo lakini tunaendelea kuwasiliana na wenzetu wa Mwanza ili waweze kufika eneo ambalo mtoto analitaja na anapafahamu hadi nyumbani kwao,”alisema.

Kuhusu hali yake ya Macho alidai kwa mujibu wa daktari aliyemfanyia uchunguzi alidai kama atapata matibabu mazuri huenda akapona ,lakini jicho moja alidai limeishaharibiwa vibaya na pilipili huenda lisipone kabisa.

“Kwa sasa tumemuhifadhi kwenye kituo cha kulelea watoto wa mazingira magumu cha Jol Centre kwa muda kwa kuwa hatuna sehemu ya kuwahifadhi hawa watoto wakati tukisubiri wazazi kama watapatikana”alibainisha.

Alisema dawati lao kwa sasa linakusudia kuanzisha kliniki kwa ajili ya kuwashughulikia watoto na kutoa elimu kwa wazazi waweze kutoa taarifa mapema ili kuhakikisha ukatili kwa watoto unapungua.

No comments: