Baadhi ya wakulima wa Tumbaku wilayani Sikonge mkoani Tabora wakifunga tumbaku yao kwa ajili ya kuikausha. |
Nyumba ya mkulima wa Tumbaku wa Chama cha Msingi Ugunda iliyopo Kijiji cha Makazi kata ya Ipole wilayani Sikonge |
Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika maeneo mbalimbali kata ya Ipole,wakulima hao pamoja na kulalamikia vitendo vya rushwa vinavyofanywa na Wachambuzi hao kwa wakulima ili waweze kupitisha katika soko tumbaku yao,walibainisha kuwa Chama Kikuu Cha Ushirika wa Wakulima wa zao hilo kanda ya Magharibi WETCU kimekuwa hakiwasaidii wakulima wanapokumbwa na matatizo mbalimbali yakiwemo ya kushuka bei kwa zao hilo pamoja na kupandishwa kiholela bei za pembejeo.
Kwaupande wake Bi.Tabu Rajabu ambaye pia ni mkulima wa zao hilo tangu mwaka 1970 alisema kwasasa hakuna wanachokipata kutokana na zao hilo na hasa wakati huu ambao wamekuwa wakibabaishwa katika mfumo wa ununuzi wa kutumia fedha za kigeni(Dola)
''Sisi hatujui hiyo Dola inabadilishwaje mradi tunaandikiwa hundi tunakwenda kuchukua pesa benki,sasa kama tukikuta ni ndogo hatuna mtu wa kumlalamkia"alisema Tabu
Pamoja na kutumia vyama vyao vya msingi kama mkombozi wao katika zao hilo upande wa manunuzi lakini pia wamekuwa wakigonga mwamba kutokana na ukweli kwamba viongozi wa vyama hivyo hawana namna ya kufanya kwakuwa nao pia wapo chini ya WETCU.
No comments:
Post a Comment