MBUNGE WA JIMBO LA SERENGETI ATAKA MAAFISA WA USALAMA WAFIKISHWE MAHAKAMANI HARAKA,
Na Anthony Mayunga-Serengeti
Machi 29,2012.
MBUNGE wa jimbo la Serengeti Dk,Stephen Kebwe ameitaka serikali
kuwachukulia hatua maafisa wa usalama waliokamatwa ndani ya hifadhi
wakichimba dhahabu kwa kuwafikisha mahakamani mara moja kama raia
watano kwa kuwa kosa lao ni moja.
Machi 23 mwaka huu aliyekuwa kamanda wa polisi wilaya ya Serengeti
Paulo Mng’ong’o ,afisa usalama wa taifa Said Mussa ,dreva wa polisi
koplo Frematus na raia watano walikamatwa ndani ya hifadhi ya
Serengeti eneo la kilima fedha wakituhumiwa kuchimba dhahabu kinyume
cha sheria.
Akiongea na mwandishi wetu kwa njia ya simu kutokea Dar es Salaam kwenye
vikao vya kamati za bunge Dk,Kebwe alisema kuwa kitendo hicho hawezi
kukifumbia macho na kuwa atahakikisha anafuatilia ili kuhakikisha na
wao wanafikishwa mahakamani kama wenzao.
“Kwa mujibu wa katiba kazi ya bunge ni kuisimamia serikali,kwa hili
nasema sitarudi nyuma maana tulidhani tuna viongozi wanaolinda
raslimali zetu kumbe wanapora ,sasa wanahamishwa ili kutudanganya kwa
madai uchunguzi unaendelea,hao wengine umekamilikaje wakafikishwa
mahakamani lakini wao unaendelea,lazima washitakiwe”alisema kwa
msisitizo.
Alidai kushangazwa na uamuzi wa siku ya tukio maafisa hao kuachiwa
usiku saa 8,”serikali gani inakuwa kazini hadi saa 8 usiku kisha itoe
dhamana ,huu ni ujanja ambao hatuwezi kuulea na watu wakazidi kulaumu
serikali ya awamu ya nne”alidai Mbunge.
“Sikutegemea kusikia kuwa maafisa hao wako nje bado wakati wenzao wako
mahabusu ,ndiyo maana magereza yamejaa wanyonge tu wakubwa wanafanya
ufisadi wao wanalindwa ,tukio hilo ni mfano halisi”alisema.
Aliahidi kukutana na waandishi wa habari kuzungumzia suala hilo hivi
karibuni kwa kuwa maafisa hao wametenda makosa ya jinai ambayo
hawatakiwi kubebwa hivyo kwa kuwa hawako juu ya sheria na ikizingatiwa
kuwa eneo walilokutwa lilivyo nyeti na wao ndio walipaswa kulinda
badala yake wanashiriki kuhujumu.
“Kuwapeleka Musoma ama kwingineko ndiko wanataka waharifu kama hao
,wanatakiwa kushitakiwa wajibu mashitaka yanayowakabili,nasema tena
kama ilivyo kwenye ibara ya 63(2) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ya mwaka 1977 nalifuatilia,”alibinisha.
Ibara ambayo inabainisha kuwa Sehemu ya pili ya Bunge itakuwa ndicho
chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka ,kwa
niaba ya wananchi ,kuisimamia na kuishauri serikali ya Jamhuri ya
Muungano na vyombo vyake katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mjibu
wa katiba hii.
Kauli hiyo kali ya mbunge inakuja siku moja tu baada ya Mwenyekiti wa
shirika lisilo la kiserikali la Wasaidizi wa Kisheria na Haki za
Binadamu wilayani Serengeti(Washehabise)kutaka sheria kutoa taarifa
kwa wananchi nini kinaendelea dhidi ya maafisa hao kutokana na tuhuma
zinazowakabili.
Machi 23,mwaka huu maafisa hao wakiwa na raia watano ambao
wameishafikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mfawidhi wa wilaya
kwa makosa matano na kunyimwa dhamana walikamatwa eneo moja la Kilima
fedha ndani ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti wakichimba dhahabu.
Raia hao walidai kuwa walipelekwa na maafisa hao kwa gari la polisi PT
1862, wakiwa wamefungiwa ndani ya turubai wakiwa na bunduki aina ya
Smg na bastola ,milipuko,koleo,nyundo,sururu,viroba 10 vya mchanga wa
dhahabu,huku getini waliandikisha wanaenda Serena kikazi.
Raia waliofikishwa mahakamani machi 26 ni Mniko Nyamhanga(30)Jonas
Marwa(42)Maiga James Maganjala(26)Mwita William na Alex Peter Mabu
ambao walisomewa mashitaka ya kuingia hifadhini,
Kupatikana na siraha bila kibali,kufanya uchimbaji wa dhahabu eneo la
hifadhi ,kukutwa na mifuko 10 ya mawe yanayodhaniwa kuwa ya dhahabu
,na kupatikana na vifaa vya milipuko ndani ya hifadhi,walikana
mashitaka na wako mahabusu hadi april 10,2012 kesi hiyo itakapotajwa
tena.

No comments:
Post a Comment