Pages

KAPIPI TV

Thursday, March 29, 2012

WAFUGAJI WAMTWANGA RISASI MGAMBO WA KIJIJI"Kisa alizidisha kuwakamata mara kwa mara,Mtendaji naye afyatuliwa risasi mara mbili lakini zikamkosa""

Watu wawili wanaodaiwa kuwa ni wafugaji wa kijiji cha Keza tarafa ya Ulyankulu wilayani Urambo mkoani Tabora wamemfyatulia risasi na kumjeruhi vibaya mgambo wa kijiji hicho kwa  lengo la kutaka kumuua.

Kwa mujibu wa maelezo ya mgambo huyo ambaye amefahamika kwa jina la Masai Mwandu(44)mkazi wa kijiji cha Keza,alidai kuwa tukio hilo limetokea hatua chache kutoka nyumbani kwake muda mfupi mara baada ya kuwasindikiza wageni waliokuwa wamekuja kumtembelea majira ya saa tatu usiku.

Masai ambaye kwasasa amelazwa katika hospitali ya mkoa wa Tabora Kitete alisema wakati akirejea nyumbani baada ya kuachana na wageni wake,ghafla alishtukia watu wawili (majina tunayo)waliibuka kutoka nyuma ya mti uliokuwa pembezoni mwa barabara na kumfyatulia risasi iliyompata kwenye mapaja miguu yote miwili.

"Nilianguka chini na kuanza kupiga kelele ya kuomba msaada kwa familia yangu,nilikuwa nikiagiza waniletee bunduki yangu ili nipambane nao licha ya kuwa tayari nilikuwa siwezi hata kusimama"alisema Masai

Hata hivyo pamoja na kelele zote za mayowe aliyopiga lakini hakukuwa na mtu aliyemsaidia hadi alipopata fursa ya kujikokota mwenyewe kwa kutambaa hadi nyumbani kwake,ndipo majirani na familia kwa ujumla wakajitokeza kumuwahisha hospitali kwa ajili ya matibabu.

Kwaupande mwingine kuhusiana na tukio hilo Mgambo huyo alifafanua kisa cha yeye kutendewa unyama na wafugaji hao ni kutokana na shughuli za kiusalama kijijini hapo ambapo wamekuwa wakiwakamata baadhi ya waharifu ambao ni  jamaa zao wa karibu na watu hao waliohusika na  tukio hilo.

Alisema kumekuwa na vitisho dhidi yake pamoja na mtendaji wa kijiji hicho cha Keza Bw.Paschal Anthony ambaye kuna taarifa ya kukoswakoswa na risasi zaidi ya mara mbili mfululizo katika matukio mawili tofauti.

"Risasi walizonifyatulia mimi zilikuwa ni za kienyeji zinazotumika kwa bunduki aina ya Gobore kama walivyofanya kwa mtendaji wa kijiji ambaye tunashirikiana kikazi.     

No comments: