WANAHARAKATI WATAKA MAAFISA WA USALAMA WALIOKAMATWA WAKICHIMBA
DHAHABU WAFIKISHWE MAHAKAMANI.
Na Anthony Mayunga-Serengeti
Machi 28,2012.
Siku moja tu baada ya kamanda wa polisi mkoa wa Mara Robert Boaz
kutangaza uamzi wa kuvuliwa madaraka aliyekuwa kamanda wa polisi
wilaya ya Serengeti Mratibu Mwandamizi wa polisi Paulo Mng’ong’o
kutokana na kukamatwa hifadhini ,Wanaharakati wameibuka na kutaka
waliohusika wote washitakiwe haraka.
Kuibuka kwa kundi hilo kunakuja huku tayari aliyekuwa kamanda wa
polisi wilaya(OCD) amevuliwa madaraka na kuhamishiwa Musoma chini ya
kamanda wa polisi wa mkoa,huku afisa usalama akikabidhi vitu vya
ofisi,na raia watano wakiwa wamefikishwa mahakamani.
Mwenyekiti wa shirika lisilo la kiserikali la Wasaidizi wa Kisheria na
Haki za Binadamu wilayani Serengeti(Washehabise)Samweli Mewama
akiongea na Mwananchi alisema wananchi wanataka kuona wanafikishwa
mahakamani kama watuhumiwa wengine waliokamatwa nao.
“Ni tendo la hatari kama maafisa hao wanaendelea kuwa kazini wakati
wenzao wako mahabusu ,kwa kuwa kitendo chao cha kuingia hifadhini
kuchimba dhahabu tena wakiwa na gari,bastola,Smg na nguo za serikali
hakina tofauti na ujambazi ama ujangili,lazima wafikishwe mahakamani
kujibu tuhuma”alisema.
Mewama alisema kuwa wanauzoefu wa askari wakikosa huhamishwa kupisha
uchunguzi lakini hakuna hatua zinazochukuliwa,”mwaka jana askari
wametuhumiwa kuua watu watatu hapa ,waliohusika wakahamishwa lakini
wako kazini ,hata hawa ambao kwanza walitakiwa kuwa mahabusu
wametolewa wanapelekea akina nani wanaotaka waharifu?”alihoji.
Alisema kauli za viongozi akiwemo Rais Jakaya Kikwete na Igp Saidi
Mwema ya kusafisha jeshi hilo hazina maana kama zinagusa wadogo kama
ilivyotokea kwa askari aliyeingia disco na bunduki huko Moshi
alifukuzwa kazi,na kuwa hana tofauti na hao walikamatwa wakiwa na
bunduki wakichimba dhahabu.
Adai mtandao huo unahusiana na majangili.
Ongezeko la uwindaji wa tembo kwa kutumia siraha za kivita unaashiria
wazi kuwa wahusika walikuwa na mtandao na wahusika ,ndiyo maana siraha
zinaingia kwa kasi wilayani humo licha ya kutangaza kuwa zimerudishwa
nyingi.
“Nimewahi kusema wale walikamatwa na siraha wafikishwe mahakamani
viongozi wakashikwa na kigugumizi matokeo yake alifikishwa diwani wa
kata ya Machochwe Samweli Gibewa kutokana na tofauti ya kisiasa
,wengine wote walikuwa wanamalizana polisi wanaandikiwa wamerudisha
kwa hiari wakati tuna taarifa walikamatwa waliteswa wakakaa
mahabusu,”alisema.
Alisema hata mauaji ya Faru George askari wa Tanapa walisema bunduki
iliyohusika ni ya kijeshi,”nilimuuliza huyo Ocd kwanini wanaua raia
wakidai waliua faru wakati siraha inatajwa ni ya kijeshi
akanikoromea,sasa kakamatwa mwenyewe porini je kama anaujasiri wa
kwenda kuchimba hifadhini anashindwaje kuua faru ama tembo maana wao
shida ni fedha “alibainisha.
Aliitaka serikali kuwa makini na watu inaowapeleka wilayani humo
kutokana na kuwa kuna vishawishi vingi,kwa kuwa wanaoharibu kwingine
wamekuwa wakipelekwa humo kama adhabu nao badala ya kutimiza wajibu
huendeleza ubaya wao,na kuomba uchunguzi wa kina ufanywe hapo polisi
maana mtandao huo ni mkubwa.
“Wananchi wamefikia hatua ya kutotoa taarifa polisi labda mtu
amekufa,maana wakifika wanaombwa mafuta ,wakati mafuta ya serikali
yapo yanatumika kwenda kuchimba dhahabu,hata mahabusu wanasombwa na
magari mabovu ya watu kuhararisha yaendelee kutembea wakati gari
linafanya kazi za watu binafsi,”alisisitiza Mewama.
Afisa usalama akabidhi.
Said Mussa ambaye ni afisa usalama wa taifa wilaya amekabidhi vifaa
vya ofisi na haiingii ofisini akisubiri hatima yake mwananchi
imebaini.
Habari za uhakika zinadai kuwa mbali na kukabidhi vifaa vingine
ikiwemo gari,afisa huyo alikabidhi siraha aina ya bastola ambayo
inadaiwa kuwa hatua ya mwisho kukabidhi na kuashiria kuwepo kwa hatua
kubwa dhidi yake.
Habari zinasema kuwa wakati wowote anatarajiwa kuingia afisa mwingine
kushika nafasi yake,wakati huohuo Mng’ong’o ameishaenda Musoma kama
ilivyoamriwa kwa ajili ya hatua zaidi za kinidhamu baada ya kumvua
madaraka yake,lakini dreva wa gari la polisi koplo Frematusi bado yuko
kazini licha ya kunyang’anywa gari.
Timu ya uchunguzi.
Timu ya uchunguzi wa tukio hilo itakayohusisha askari polisi,usalama
wa taifa na Tanapa inategemewa kuanza na kumaliza kazi yake haraka ili
kutoa fursa ya hatua za kuchukuliwa dhidi ya maafisa hao kama
watabainika walihusika.
Tanapa wasisitiza hatua zichukuliwe.
Mkurugenzi mkuu wa Tanapa Allan Kijazi alisisitiza kuwa msimamo wao ni
kuhakikisha wahusika wote wanachukuliwa hatua za kisheria kwa kuwa huo
ni uharifu sawa na uharifu mwingine.
Machi 23,2012 maafisa hao wakiwa na raia watano Mniko Nyamhanga mkazi
wa Matare,Jonasi Marwa mkazi wa Mugumu mjini,Maiga Maganjala mkazi wa
Nyamakokoto wilayani Bunda,Mwita William King’eti mkazi wa Mugumu na
Alex Peter Mabu Mwalimu wa sekondari Kambarage walikamatwa ndani ya
hifadhi ya Serengeti katika eneo la Kilima fedha wakichimba dhahabu.
Walikamatwa na viroba 10 vya mawe ya dhahabu,vifaa vya
milipuko,mtambo wa kupimia dhahabu,nyumdo,sururu,pochi la kuchimbia na
sepetu.
Raia hao watano tayari wamefikishwa mahakama ya hakimu mkazi mfawidhi
wilaya Afred Kahimba wakishitakiwa kwa makosa matano,ambayo ni kuingia
ndani ya hifadhi bila kibali.
Kupatikana na siraha bila kibali,kufanya uchimbaji ndani ya hifadhi
bila kibali,kupatikana na mifuko 10 ya mawe ya madini yanayodhaniwa
kuwa ni dhahabu,kukutwa na vifaa vya milipuko.wote walikana mashita
wako mahabusu hadi aprili 10,2012.

No comments:
Post a Comment