Watu wasiojiweza wanaoishi katika kijiji cha Amani manispaa ya Tabora wamejikuta katika hali ambayo hawakutarajia ya kukosa chakula hata kufikia hatua ya kupitisha siku nzima pasipo kupata hata mlo mmoja.
Wakizungumza na mtandao huu ambao ulifika katika kijiji hicho kwa lengo la kutaka kujua matatizo yanayowakabili ambapo baadhi ya walemavu walionesha kukata tamaa ya kupata msaada kwa siku za hivi karibuni ili kukidhi mahitaji ya maisha yao ya kila siku.
Bw.Maganga Shaban mmoja kati ya wakazi wa kijiji hicho cha Amani pamoja na kuthibitisha mara ya mwisho wa kupokea msaada wa chakula toka serikalini mwanzoni mwa Januari lakini kwa sasa hali imekuwa ngumu na hasa wale wenye upungufu wa viungo vya miili yao ambao hawawezi kwenda mitaani kuomba chakula na misaada mingine ya kibinadamu.
Alisema wakati mwingine msaada unaoletwa na Serikali kupitia idara ya ustawi wa jamii umekuwa pia una matatizo kwakuwa inafikia hatua ya kuletewa chakula kibovu na kulazimika wakitumie kwakuwa hawana njia yeyote ya kupata riziki yao ya kila siku.
''Kwakweli kwasasa mimi naona hata hiyo Serikali iache kuleta hata hicho chakula ili tufe tupungue''alisema mmoja wa wakazi wa kijiji hicho aliyefahamika kwa jina la Masanja ambaye ni mlemavu wa miguu na pia haoni.
Hata hivyo walemavu hao wamesifia viongozi wa makanisa mbalimbali hapa mkoani Tabora kwa michango yao licha ya kuwa si ya mara kwa mara lakini imekuwa ikiwasaidia na kwamba huwa hawatoi kwa masimango.
Kwaupande mwingine baadhi ya walemavu hao wamemuomba mkuu wa mkoa wa Tabora Bi.Fatma Mwassa kufanya ziara ya ghafla katika kijiji hicho ambacho ni kambi ya kuhifadhi watu wasiojiweza kinachomilikiwa na Serikali ili aje ajionee maisha ya watu hao ambao ni watanzania wenye haki ya kupata maisha bora.
''Pamoja na kuonekana watu wasiojiweza wamezagaa mjini na kuendelea na shughuli za kuombaomba lakini kuna haja kwa jamii kuangalia uwezekano wa kunusuru maisha ya watu hawa,nalisema hili liwe ni changamoto kwa serikali na wananchi kwa ujumla''alisema mmoja wa wakazi wa Tabora mjini ambaye hakutaka jina lake litambulike katika hadhara.

No comments:
Post a Comment