Pages

KAPIPI TV

Wednesday, March 28, 2012

MAMA AMCHOMA MOTO MKONONI MTOTO WAKE"Kisa eti alikomba mboga,ashindwa kuandika darasani,walimu na mtendaji wampeleka Polisi"

Mtoto Nyamizi Charles akisindikizwa kituo cha Polisi Isevya na mtendaji wa kata ya Isevya Bw.Revocatus Rugeiyam pamoja na mmoja wa walimu wa shule ya msingi Bombamzinga.
Bi.Joha Aman(40)mama mzazi wa mtoto Nyamizi Charles
Mwanafunzi wa darasa la kwanza shule ya msingi Bombamzinga, Nyamizi Charles(10) akiwa amefika kituo cha kidogo cha Polisi Isevya Manispaa ya Tabora kufuatia tukio la kuchomwa moto mkononi na mama yake mzazi Bi.Joha Amani.

 Katika hali isiyo ya kawaida mtoto Nyamizi Charles(10)ambaye ni mwanafunzi wa darasa la kwanza shule ya msingi Bombamzinga manispaa ya Tabora amechomwa moto na mama yake mzazi anayefahamika kwa jina Joha Amani(40)mkazi wa Kata ya Isevya mtaa wa Kazima kwa madai ya kukomnba mboga.

Akisimulia tukio hilo la kuhuzunisha ambalo lilikuwa na mtazamo kama mchezo wa kuigiza,mtendaji wa kata ya Isevya Bw.Revocatus Rugeiyam alisema,mtoto huyo ambaye aliletwa ofisini kwake na walimu wake wakidai kuwa mtoto huyo amejeruhiwa kwa kuchomwa moto na mama yake.

Kwamujibu wa mtendaji huyo walichukua uamuzi wa kumfuata mama mzazi wa mtoto huyo Bi.Joha Amani na kumchukua hadi kituo cha Polisi Isevya ambako mama huyo aliendelea na msimamo wake kuwa alikuwa ana mwadabisha mtoto huyo na hakuna mtu wa kumwingilia katika maamuzi hayo.

Pamoja na kuwekwa ndani katika kituo hicho Bi.Joha aliendelea kulalamikia askari wa kituo hicho kwa kumweka ndani.

Kwaupande mwingine chanzo cha walimu wa shule hiyo ya Bombamzinga kugundua unyama aliofanyiwa mtoto huyo ni pale mwalimu wa darasa la kwanza Bi.Zulfa Kondo alipomwambia aandike kama ilivyo ada kwa wanafunzi wengine lakini Nyamizi alishindwa na hivyo mwalimu akawa amegundua hali hiyo iliyosababishwa na majeraha aliyokuwa nayo mkononi.

Mkuu wa shule hiyo Bw.Peter Sizya alipata taarifa kutoka kwa mwalimu wa darasa ambalo anasoma mtoto Nyamizi na hivyo kufanya uamuzi wa kwenda ofisi ya mtendaji wa kata.

Hata hivyo matukio ya unyanyasaji kwa watoto wadogo hapa mkoani Tabora yamekuwa yakifanyika mara kwa mara ingawa yapo yanayoripotiwa na mengine yanapita kimya kimya.     




No comments: