Pages

KAPIPI TV

Tuesday, March 27, 2012

TBL YAOMBWA KUSAIDIA MIRADI YA MAJI VIJIJINI TABORA"Uzinduzi wa muonekano mpya radha ile ile''

HIVI NDIVYO MAMBO YALIVYOKUWA FRANKMANN HOTEL TABORA
Meya wa Manispaa ya Tabora, Bw.GHULAM DEWIJ na Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP ANTHONY RUTHA wakati wa uzinduzi wa muonekano mpya radha ile ile.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Tabora Bw.Ghulam Dewij pamoja na maafisa wa TBL wakicheza muziki wa Dansi uliokuwa ukitumbuizwa na Bendi ya Frankmann ya mjini Tabora.

Mstahiki meya wa manispaa ya Tabora Bw.Ghulam Dewij ameiomba kampuni ya bia nchini TBL kuangalia uwezekano wa kusaidia miradi ya maji vijijini hali ambayo itazidi kudhihirisha uwajibikaji wa kampuni hiyo kwa umma wa watanzania.


Bw.Ghulam ametoa rai hiyo wakati akihutubia katika uzinduzi wa Muonekano Mpya wa bia ya Balimi ikiwa na radha ile ile katika ukumbi wa Frenkmann Hotel mjini Tabora.

Kwa upande wake Meneja masoko wa TBL kanda ya magharibi Bw.Robert Kazinza alisema kampuni hiyo imeamua kubadilisha muonekano wa bidhaa hiyo ya Balimi ambayo ni kinywaji kinachokubaliwa na wengi hususani wakulima kama ilivyo jina la kinywaji hicho.

''Tayari tumekwisha fanya uzinduzi katika mikoa ya Mwanza,Shinyanga na sasa Tabora na pia tunaendelea Kigoma kwakuwa kinywaji hiki ni kwa ajili ya wananchi wa kanda hii ya Magharibi na kwakweli ni Fahari yao"alisema Kazinza wakati alipokuwa akitambulisha kinywaji hicho cha Balimi Extra.


Katika hafla fupi iliyofanyika jana usiku na ilihudhuriwa na wadau mbalimbali wa kinywaji cha Balimi akiwemo mkuu wa wilaya ya Tabora Bw.Moshi Chang'a,kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora,baadhi ya wafanyabiashara,watumishi wa serikali,waandishi wa habari pamoja na wanachuo wa chuo cha utumishi wa umma TPSC tawi la Tabora.  
















No comments: