Pages

KAPIPI TV

Tuesday, March 27, 2012

OCD WA SERENGETI AVULIWA MADARAKA"Ni kutokana na madai ya tuhuma za kukutwa wakichimba dhahabu ndani ya hifadhi ya Taifa''


Na Anthony Mayunga-Serengeti
Machi 27,2012.

MKUU wa jeshi la polisi Tanzania Said Mwema ametengua uteuzi wa
kamanda wa polisi wilaya ya Serengeti  Mrakibu Mwandamizi wa polisi
Paulo  Mng’ongo kutokana na tuhuma za kukutwa ndani ya hifadhi ya
Taifa ya Serengeti akihusishwa na uchimbaji wa madini aina ya dhahabu.

Machi 23.2012 kamanda huyo,afisa usalama wa taifa wilaya Said Musa
,dreva wa polisi ,na watu wengine watano walikamatwa wakiwa ndani ya
hifadhi ya taifa ya Serengeti ambako kuna machimbo ya dhahabu ya
kilimafedha yaliyohifadhiwa.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mara Robert Boaz alisema kutokana na tuhuma
zinazomkabili ,”aliyemteua
ameamua kutengua uteuzi wake kuanzia machi 25,mwaka huu na atakuwa
mkoani hapa wakati uchunguzi ukiendelea”alisema.

Alisema kwa dereva wa gari la polisi yeye atashughulikiwa akiwa kituoni
kwake kutokana na ngazi yake,huku akikwepa kuzungumzia afisa usalama
wa taifa kwa madai kuwa wakuu wake ndio wanatakiwa kuchukua hatua za
kinidhamu dhidi yake.

“Mimi nazungumzia walioko chini yangu hiyo ni mamlaka nyingine lakini
kwa vyovyote hatua za kinidhamu lazima zitachukuliwa”alisema.

Timu ya uchunguzi yaundwa.
Kamanda Boaz alisema ili kupata ukweli wa tukio na sheria iweze
kuchukua mkondo wake wameunda timu ya uchunguzi itakayowahusisha
Polisi,Usalama wa taifa na Tanapa.

Hata hivyo hakuwa tayari kusema muda wa uchunguzi,”kwa ujumla hatujui
uchunguzi utakamilika lini”siwezi kusema lini uchunguzi utakamilika
lakini nategemea utafanyika kwa haraka sana”alisema.

Azungumzia tukio.
Alisema maafisa hao walikutwa wameegesha gari lao pembeni mwa eneo la
machimbo ndani ya hifadhi paitwapo Kilima fedha ,lakini walidai kuwa
walikuwa kikazi eneo hilo.

“Walichukuliwa na kupelekwa Seronera lakini askari wa Tanapa
waliendelea kufanya doria eneo hilo,lakini saa 7 mchana watu watano
walitoka ndani shimo na viroba 9 vya mchanga wenye dhahabu ,vifaa vya
kuchimbia ,milipuko na mtambo wa kupimia dhahabu.

Walipoulizwa walisema kuwa walikuwa na maafisa hao kuwa ndio
waliowaleta eneo hilo ,walikamatwa na kupelekwa Seronera na
kuunganishwa na maafisa hao.

Wakati hayo yanatokea Ocd huyo alikuwa na uhamisho wa kwenda mkoani
kuwa msaidizi wa kamanda wa polisi wa mkoa wa Mara,na kuwa mwezi juni
alitakiwa kuripoti kituo chake kipya na kutumikia nafasi hiyo

Waliokamatwa.
Mniko Nyamhanga Mwita(30)mkazi wa Matare ,Jonas Marwa Chacha (42)mkazi
wa Mugumu mjini,Maiga James Majanjala(26)mkazi wa Nyamakokoto Bunda
ambaye alikuwa na mtambo wa kupimia dhahabu na amefanya kazi kwenye
machimbo ya Majimoto.

Wengine ni Mwita William King’eti (30)kazi wa Mugumu na Alex Peter
Mabu(29)Mwalimu wa sekondari Kambarage iliyoko mjini Mugumu,ambao wote
wamefikishwa mahakamani.

Hata hivyo imeshuhudiwa aliyekuwa kamanda wa polisi wilaya Mng’ong’o
akipakia mzigo yake kwenye gari la polisi PT 1862 kwa ajili ya kwenda
Musoma na aliyekaimishwa nafasi hiyo ni mkuu wa upelelezi wa makosa ya
jinai wilaya.

Wananchi waomba haki itendeke.
Ili kuhakikisha vitendo vya uharifu vinavyoongozwa na vyombo vya dola
wananchi wilayani hapa wanaomba watuhumiwa washughulikiwe kama
waharifu wengine,na kusiwepo tabia ya kulindana.

“Mambo mengi yanafanywa na polisi ikiwemo mauaji kwa raia lakini
hakuna hatua zinazochukuliwa,hili wamekamatwa askari wakubwa tutegemee
nini kama matukio mengi hawashiriki?”alisema mmoja wa wananchi jina
tunalo.

Wahusishwa na mtandao wa ujangili.
Baadhi ya skari wa hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambao hawakupenda
majina yao kutajwa walisema ongezeko la ujangili lina uhusiano wa
karibu na maafisa wa vyombo vya usalama.

“Mnakamata jangili na meno ya tembo na bunduki mkiwafikisha polisi
kesho mnawakuta mitaani ,au mnawakamata tena kwa matukio hayohayo
,lakini unawakuta na maafisa hao mara kwa mara ,tunahangaika sana
kulinda maliasili hizi lakini wengine ni dill”walisema.













No comments: