Watu kumi akiwemo mwanamke mmoja wamefikishwa mahakama ya hakimu mkazi mjini Tabora kwa mara ya kwanza kufuatia kuhusika na tuhuma za mauaji ya aliyekuwa mwenyekiti wa halmashauri ya Uyui marehemu Mashaka Hassan Kalyuwa.
Watuhumiwa hao ambao miongoni mwao tisa, mbele ya hakimu mkazi Bw.Hamisi Bally wamefunguliwa shitaka la kesi namba tano la mwaka 2012 ambalo linalobainisha kuwa mtuhumiwa namba moja Bw.Omela Nchoji pamoja na wenzake wanadaiwa kumuua Mashaka Hassan Kalyuwa kwa kumpiga risasi.
Sambamba na kesi hiyo watuhumiwa wengine saba miongoni mwao wamefunguliwa kesi ya kumiliki silaha aina ya Shortgun na Gobore pamoja na risasi tatu kinyume cha sheria ambapo kesi hiyo ndiyo inayomuhusisha mwanamke huyo anayefahamika kwa jina la Hadija Jumanne.
Aidha kesi hiyo kwa mujibu wa taratibu za mahakama watuhumiwa walielezwa kuwa mahakama hiyo ya hakimu mkazi haina uwezo wa kisheria wa kusikiliza na kutoa maamuzi ya kesi hiyo hivyo watasubiri wakiwa mahabusu hadi hapo itakapo anza kusikilizwa na mahakama kuu kanda ya Tabora ingawa tarehe 10 April 2012 itatajwa tena huku ikiwa inasubiri uchunguzi wa kutoka jeshi la Polisi.
No comments:
Post a Comment