Mwanafunzi wa Shule ya Bombamzinga akionesha dharau mbele ya wazazi na wajumbe wa bodi ya Shule hiyo hali iliyofanya hata baadhi ya wanafunzi wenzake wamshangae. |
Baadhi ya kundi la wanafunzi wa shule hiyo ambao wanatuhumiwa kujihusisha na vitendo viovu na hasa kutishia kuwapiga walimu na wanafunzi wenzao |
Wajumbe wa bodi ya shule wakiwa na baadhi ya wazazi wa watoto hao watukutu wakijaribu kutafuta suluhu |
Mkuu wa Shule ya sekondari Bombamzinga Bw.Victor Nkana. |
Kikao cha bodi ya shule ya sekondari ya Bombazinga iliyoko
manispaa ya Tabora kimeridhia kufukuzwa shule wanafunzi wawili wa kidato cha pili
Masoud Seleman na Daniel Fares kwa kuwapiga na kutishia kuwaua walimu wa nidhamu na ulinzi katika shule hiyo.
Ilielezwa katika kikao hicho kilichohudhuriwa pia na baadhi
ya wazazi wa wanafunzi watovu wa nidhamu kuwa, mwanafunzi huyo Masoud Seleman
ambaye ni maarufu kwa jina Gadaf mbali na kumtishia kumuua mwalimu huyo wa
nidhamu Bw.Majaliwa Damiani,amekuwa na vitendo vya kuwapiga baadhi ya wanafunzi
na kuwasababishia majeraha huku mwanafunzi Daniel Fares alimpiga ngumi mwalimu wa ulinzi Bw.Kategile na kumsababishia maumivu.
Sambamba na hilo maelezo yaliyotolewa na mkuu wa shule hiyo
ya sekondari ya Bombamzinga Bw.Victor Nkana yaliweka bayana katika kikao hicho
kuwa Mwanafunzi huyo Masoud(Gadaf)amekuwa ni mtovu wa nidhamu tangu alipoingia
shuleni hapo yeye pamoja na wanafunzi wengine wapatao thelathini.
Aidha kwa upande mwingine alieleza kuwa Masoud imethibitika
kuwa mbali na uvutaji bangi amekuwa akiandika matusi katika karibu majengo yote
ya shule hiyo na kusababisha uongozi wa shule kuingia gharama ya kupaka rangi
majengo ya shule nzima.
Hata hivyo pamoja na mwanafunzi huyo kubainika kufanya uovu
huo na kuomba pesa ya bhangi kwa nguvu kwa wapita njia kwa kushirikiana na
baadhi ya vijana wengine ambao si wanafunzi wa shule hiyo,uongozi wa shule
ulimwita mzazi wa Masoud ili kumweleza uovu anaoufanya Masoud lakini mzazi
hakuwa tayari kufika shuleni hapo.
Kwaupande mwingine Masoud Seleman akiwa na wanafunzi wenzake
wapatao kumi na watano wakiwa na silaha marungu na visu, walivamia jengo la
utawala shuleni hapo kwa lengo la kutaka kumkomboa mwenzao aliyekuwa anatumikia
adhabu yake ya kufanya usafi kwenye jengo hilo
la utawala.
Bodi ya shule ya Bombamzinga imetoa onyo kali kwa wanafunzi
wapatao thelathini watovu wa nidhamu wakiwemo washirika wenza wa Masoud mbele
ya mwakilishi wa Afisa Elimu mkoa wa Tabora Bw.Alfred Kafuku,kutorudia makosa
wanayoyafanya wakiwa shuleni na hata nje ya Shule.
No comments:
Post a Comment