Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Anthony Rutha akiwaonesha waandishi wa habari mtambo wa kutengenezea bunduki za kienyeji zinazotumika katika shughuli za ujambazi mkoani Tabora na mikoa jirani. |
Baadhi ya vidhibiti zikiwemo simu za marehemu Mh.Mashaka Kalyuwa pamoja na silaha zinazodaiwa kutumika kufanya mauaji hayo. |
Jeshi la Polisi mkoani Tabora linawashikilia watu tisa kwa
tuhuma za kuhusika na mauaji ya aliyekuwa mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya
ya Uyui Mh.Mashaka Kalyuwa.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Anthony Rutha alisema tukio la mauaji hayo lilitokea mnamo tarehe 2/3/2012 majira ya saa moja na
nusu usiku ambapo watuhumiwa hao tisa kila mmoja kwa nafasi yake walihusuka
kufanya mauaji hayo katika kata ya Ipuli manispaa ya Tabora.
Aidha kamanda Rutha alifafanua mbele ya waandishi wa habari
ofisini kwake leo hii asubuhi kuwa watuhumiwa wakiwa na silaha mbalimbali
bunduki za kienyeji zinazotumia risasi za Shortgun siku hiyo walivamia nyumbani
kwa marehemu Mashaka huko Ipuli na kumkata kwa panga kichwani na baadaye kumpiga risasi iliyosababisha kifo chake.
Kamanda Rutha ameyataja
majina ya watuhumiwa waliohusika na mauaji hayo kuwa ni Omela Nchonji(40) mkazi
wa Misole,Mathias Lubiza Sumuni(38)mkazi wa Kahama,Paschal Nkinga(43)mkazi wa
Nkinga Igunga,Masoud Said Juma(41)mkazi wa kidatu Ipuli,Athuman Juma(30)mkazi
wa kidatu chini Ipuli,Paul Magale(22)mkazi wa Kahama,Mihayo Stephano(28)mkazi
wa Kiloleni,King Masanilo(31)mkazi wa Kiloleni na mwingine ni Haruna Athuman
Kidaso(42)mkazi wa Mwanzaroad Tabora mjini.
ACP Rutha alisema baada ya uchunguzi wa awali ulibaini kuwa
mauaji hayo yalifanywa na watuhumiwa hao kwa kisasi baina yao na Marehemu
Mashaka.
Kwaupande mwingine Kamanda Rutha alisema watuhumiwa
wamehojiwa na kukiri kuhusika na mauaji hayo huku akitumia fursa hiyo
kuwashukuru wananchi wa Tabora kwa ushirikiano wao katika kufanikisha kukamatwa
kwa watuhumiwa hao ambao watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.
No comments:
Post a Comment