Na Pardon Mbwate na Felister Chubwa wa Jeshi la Polisi
Kigoma
KIGOMA
JUMANNE MEI 1, 2012.
Mkazi mmoja wa Kijiji cha Katanga
katika wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma, Petro Masumbuko(37), amejeruhiwa
viabaya kwa kupigwa risasi mbavuni na majambazi kisha kupora shilingi elfu saba
na simu moja ya mkononi.
Kamanda wa Polisi mkoni Kigoma
Kamishna Msaidizi ACP Frasser Kashai, amesema kuwa tukio hilo limetokea jana
marija ya saa 2.00 usiku baada ya kundi la watu wenye silaha kumvamia Bw.
Masumbuko nyumbani kwake na kumpiga risasi kabla ya kumpora fedha hizo pamoja na
simu yake ya mkononi aina ya Nokia.
Kamanda Kashai amesema majeruhi
amekimbizwa katika hospitali ya wilaya ya Kibondo kwa ajili ya uchunguzi zaidi
wa kiafya pamoja na matibabu huku Polisi nao wakiendelea na uchunguzi na
kuwasaka watuhumiwa wa tukio hilo.
Wakati huo huo, Polisi mkoani Kigoma wameanza
uchunguzi wa kifo cha mkazi mmoja wa kijiji cha Kazegunga kilichopo katika kata
ya Msimba Bw. Riziki Issa Mahela(32), aliyekutwa huko kwenye eneo la Kahabwa
mjini Kigoma akiwa ameuawa kwa kukatwa katwa kwa mapanga kichwani na
mgongoni.
Kamanda Kashai, amesema kuwa Polisi
watatafuta chanzo na sababu za mauaji hayo na kitu kilichomfanya marehemu
asafiri kutoka katika eneo la kijijini kwake hadi katika mtaa huo ambako
ameuawa.
Huyo ni mtu wa tato kuuawa katika
mazingira ya kutia mashaka katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita ambapo watu
wengione wane waliuawa katika matukio matatu tofauti huku wawili mtu na mkewe
wakiuawa kwa tuhuma za imani za kshiirikina.
Kamanda Kashai amewaonya vikali wale wote wenye
kuchukua sheria mkononi kwa kuwazuru hata kuwaua wengine kwa sababu zozote zile
kuwa watapambana na mkono wa dola kwa vyovoyte iwavyo.
Amesema Makachero wake wamejipanga kuhakikisha
kuwa kila mtu aliyehusika katika mauaji ya mmoja wa marehemu hao kuwa ni lazima
akamatwe na sheria kuchukua mkondo wake.
Amewataka wananchi mkoani humo kuendelea kutoa
ushirikiano kwa Jeshi hilo li kusaidia kufanikisha kukamatwa wa washukiwa wote
wa mauaji hayo.
Taarifa hii imehaririwa na kusambazwa
kwenu na Inspekta Mohammed Mhina, Afisa Habari Mkuu wa Jeshi la Polisi
Zanzibar
0715 886488, 0784 886488


No comments:
Post a Comment