Pages

KAPIPI TV

Sunday, May 27, 2018

WANAKIJIJI WAUFUKIA MWILI WA MWANAUME ALIYEUA,WADAI WALICHOSHWA NA MATENDO YAKE YA UJAMBAZI

Wananchi wa kijiji cha Isalalo wilayani Nzega wakichimba shimo kwa ajili kuufukia mwili wa Mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina Mijile Peter Nsimbila ambaye anadaiwa kuuawa na watu wasiojulikana baada ya kukatwa mapanga na kisha kuchinjwa na kitu chenye ncha kali akiwa hatua chache kutoka nyumbani kwake.Wananchi hao waliamua kufukia mwili huo wa marehemu Nsimbila pasipo kumpa heshima ya kumzika kwenye kaburi kama ilivyo kwa binadamu wengine hali inayodaiwa imetokana na kuchoshwa na matukio ya uhalifu wa kupindukia aliokuwa akiufanya.
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Isalalo wakiwa pembeni wakipisha vyombo vya usalama kufanya uchunguzi wa mauaji ya mwanaume mmoja Mijile Peter Nsimbila anayedaiwa kuuawa na watu wasiojulikana ambao walifika kuvamia nyumbani kwake majira ya usiku wakati akijiandaa kulala,Watu hao ambao idadi  haijafahamika  walimkimbiza hatua chache kutoka nyumbani  kwake ndipo walianza kumshambulia kwa silaha za aina mbalimbali hadi kufikia umauti.
Kamanda wa Polisi  mkoa wa Tabora SACP Wilbroad Mutafungwa amethibitisha tukio hilo la mauaji huku akieleza uchunguzi  uliofanywa na Polisi umebaini kuwa marehemu Nsimbila alikuwa akijihusisha na matukio ya ujambazi wa kutumia silaha na kwamba Polisi bado walikuwa wakimsaka kwa udi na uvumba hadi amefikwa na tukio hilo la mauaji.Kumbuku zinaonesha hivi karibuni Marehemu Nsimbila alihukumiwa kutumikia kifungo cha miaka thelathini  baada ya kupatikana na hatia ya kufanya tukio la unyang'anyi wa kutumia silaha na kupora Pikipiki lakini alikata rufaa na kufanikiwa kuachiwa huru.



No comments: