Pages

KAPIPI TV

Monday, September 14, 2015

"NICHAGUENI NIKAWASHUGHULIKIE WANAOFANYA UBADHIRIFU WA FEDHA ZA UMMA SERIKALINI"-DR.MAGUFULI

Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Dr.John Pombe Magufuli akizungumza na umati mkubwa wa wananchi wa Tabora mjini wakati wa kampeni katika uwanja wa Aly Hassan Mwinyi ambapo Dr.Magufuli aliwaomba wananchi wamchague ili aweze kupambana na watendaji ndani ya Serikali ambao sio waaminifu wanaofanya ubadhirifu kwa fedha za umma na kusababisha kuchelewesha maendeleo.Dr.Magufuli aliweka wazi kuwa anafahamu mianya yote inayotumiwa na wajanja wachache wanaojinufaisha wenyewe kupitia rasilimali za Umma hivyo ni rahisi kwakwe kupambana na watu wa aina hiyo ili kuhakikisha kila Mtanzania ananufaika na rasilimali za Taifa.
Dr.Magufuli wakati akiingia uwanjani


Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tabora mjini Bw.Emmanuel Mwakasaka akimkaribisha Uwanjani mgombea Urais Dr.John Pombe Magufuli.
Dr.John Pombe Magufuli akimkabidhi Ilani ya CCM Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tabora mjini Bw.Mwakasaka pamoja na kumnadi mbele ya umati mkubwa wa wananchi wakati wa kampeni ya Uchaguzi mkuu katika viwanja vya Aly Hassan Mwinyi mjini Tabora

Aliyekuwa mgombea Ubunge wa Jimbo la Tabora kaskazini  kwa tiketi ya Chadema  Bw.Daud Mteminyanda akizungumza namna alivyoenguliwa kuwania nafasi hiyo  dakika za mwisho wakati wa kurejesha fomu ofisi ya msimamizi wa Uchaguzi wilaya ya Uyui,Mteminyanda ameamua kujiunga na CCM baada ya Chadema kumtosa.
Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi  Abrahaman Kinana akizungumza na umati mkubwa wa wananchi waliohudhuria katika kampeni za mgombea Urais kwa tiketi ya Chama hicho katika uwanja wa Aly Hassan Mwinyi ambapo Kinana aliwaomba watanzania kumchagua Dr.Magufuli kwakuwa ni mtu mwadilifu na mchapakazi ambaye anaweza kuliongoza Taifa na anania nzuri ya kuwasaidia Watanzania.
Kundi la Orijino Komedi lilikuwepo na kuwapatia raha watanzania katika uwanja wa Aly Hassan Mwinyi



Msanii Shilole naye alikuwa miongoni mwa wasanii waliofanya burudani zilizokuwa zikimsindikiza mgombea Urais Dr.Magufuli.





No comments: