Pages

KAPIPI TV

Monday, September 14, 2015

"MKINIPA UDIWANI NITAJENGA KITUO CHA POLISI BAADA YA MIEZI MITATU"-YUSUPH KITUMBO


Mgombea Udiwani Kata ya Cheyo Manispaa ya Tabora Bw.Yusuph Kitumbo akizungumza na wananchi wakati wa Uzinduzi wa kampeni katika kata hiyo ambapo Kitumbo pamoja na kuahidi kumaliza kero mbalimbali ikiwemo ya Ujenzi wa Kituo cha Afya na Soko lakini alisisitiza kuwa endapo akichaguliwa atajenga Kituo cha Polisi ndani ya miezi mitatu. 
Mgombea udiwani Bw.Kitumbo wakati akiingia eneo la Mkutano wa hadhara ukiwa ni sehemu ya Uzinduzi wa kampeni ambapo alifuatana na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tabora mjini Bw.Emmanuel Mwakasaka, mkutano ambao ulionesha kuwa na mvuto mkubwa kwa wananchi ambayo ulifanyika katika viwanja vya Mwanga Shop. 
Mgombea Ubunge Emmanuel Mwakasaka na mgombea Udiwani Yusuph Kitumbo wakipokelewa kwa Shangwe kubwa na baadhi ya wanachama wa CCM na wakazi wa kata ya Cheyo katika mkutano wa kampeni.


Mke wa mgombea Udiwani kata ya Cheyo Mama Kitumbo akimuombea kura mumewe kwenye mkutano wa kampeni katika viwanja vya Mwanga Shop Kata ya Cheyo.



Yusuph Kitumbo akiteta jambo  la Maendeleo  ya Kata  na mmoja wa Bibi ambaye ni mkazi wa Kata ya Cheyo wakati wa uzinduzi wa Kampeni.


Wanachama wa CCM katika picha ya pamoja na mgombea wa nafasi ya Udiwani kata ya Cheyo


Baadhi ya wadau wa Maendeleo na wakereketwa wa CCM kata ya Cheyo ambayo walikuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha sherehe za uzinduzi wa kampeni zinaendelea na kufanyika ipasavyo.

No comments: