Pages

KAPIPI TV

Saturday, September 5, 2015

MUNDE AFANYA KONGAMANO KUBWA NA WANAFUNZI WA KIKE VYUO VIKUU NA KATI TABORA

Mgombea Ubunge wa Vitimaalum  mkoa wa Tabora  kwa tiketi ya CCM Bi.Munde Tambwe akizungumza katika Kongamano la Wanafunzi wa Kike wa Vyuo vikuu na vya kati katika Ukumbi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tabora ambapo katika Kongamano hilo Wanafunzi walielezea Changamoto mbalimbali zinazowakabili ambazo ni moja ya sehemu zinazokwamisha maendeleo yao hususani ukosefu wa ajira mara baada ya kuhitimu masomo yao.
Wanafunzi wa Vyuo vikuu na vya kati wakimsikiliza kwa makini Mgombea Ubunge wa Vitimaalum Bi.Munde Tambwe wakati akihutubia ambapo pamoja na mambo mengine Wanafunzi hao walimpongeza Mgombea huyo ambaye amekuwa akiwajali kwa kuwatembelea katika vyuo vyao kutambua matatizo yanayowakabili na kujaribu kuyashughulikia.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora Bw.Hassan Wakasuvi akihutubia katika Kongamano hilo ambapo pamoja na kusikiliza kero zinazowakabili Wanafunzi hao wa vyuo aliwapongeza kwa kukiunga mkono Chama Cha Mapinduzi hususani wakati huu wa kuelekea Uchaguzi mkuu ambapo aliwataka kuwapigia Kampeni wagombea wa nafasi za Udiwani,Ubunge na Urais mahali popote wanapofanikiwa kuzungumza na wananchi huko mitaani.
Mgombea Udiwani kwa tiketi ya CCM kata ya Cheyo Manispaa ya Tabora Bw.Yusuph Kitumbo alipata fursa ya kuzungumza jambo katika Kongamano hilo aliwaomba Wanafunzi hao kukipatia ushindi Chama Cha Mapinduzi katika Uchaguzi mkuu wa mwaka huu.





No comments: