Pages

KAPIPI TV

Saturday, September 5, 2015

LOWASSA APATA MAPOKEZI MAKUBWA TABORA,HAIJAWAHI KUTOKEA KWA KIONGOZI YEYOTE ALIYETEMBELEA MKOANI HUMO

Mgombea Urais kwa tiketi ya Chadema kupitia Ukawa Bw.Edward Lowassa akizungumza na Maelfu ya Wananchi wakiwemo Wafuasi wa Vyama vinavyounda Ukawa mkoani Tabora ambapo katika mkutano huo wa Kampeni  za Uchaguzi  mkuu Wananchi wamejitokeza kwa wingi kuliko ilivyokawaida hatua ambayo wengi wao wameonesha kumuunga mkono mgombea huyo aliyewaahidi kuleta Mabadiliko makubwa ya Maendeleo  endapo kama Wananchi watampatia ridhaa ya kuongoza nchi. 
Maelfu ya Wananchi waliojitokeza kumsikiliza Mgombea Urais Bw.Edward Lowassa katika viwanja vya Town School mjini Tabora
Ummati mkubwa wa Wananchi  ukimshangilia Bw.Lowassa katika mkutano wa Kampeni za Uchaguzi mkuu
Mabango yenye ujumbe mbalimbali yalikuwa ni sehemu ya Shamrashamra za Mapokezi ya Bw.Lowassa  yaliyofanywa na Wananchi wenyewe kwa hiari zao.
Waziri mkuu wa zamani Bw.Fredrick Sumaye akizungumza na Wananchi wa Tabora mjini kabla ya kumkaribisha Bw.Lowassa kuzungumza na Wananchi hao walioonesha kuwa na shauku ya kumsikiliza mgombea Urais huyo.

Helkopta iliyomleta Mgombea Urais Bw.Lowassa katika viwanja vya Town School Tabora mjini mahali ambako mkutano huo wa kampeni ulifanyika.







No comments: