Na Magreth
Magosso,Kigoma
Kufuatia hofu ya ugonjwa wa Ebola,Serikali mkoani Kigoma imeanza kuchukua hatua za makusudi kwa kutoa elimu kwa kuwatangazia wananchi mkoani humo waweze kujihadhari na ugonjwa huo hatari kutokana na kuwepo kwa muingiliano wa watu mbalimbali kutoka nchi jirani.
Akifafanua
hilo kigoma ujiji jana mbele ya wandishi wa habari, Mkuu wa mkoani wa Kigoma kanali mstaafu Issa Machibya alisema kutokana na mwingiliano na
mahusiano ya nchi jirani za DRC-Congo na Burundi kuna uwezekano mkubwa ugonjwa huo kuingia nchini kupitia mkoani humo hali
inayolazimu kuanza kuchukua hatua za tahadhari
kwa kutoa elimu umma.
Kanali Machibya ametoa
maelekezo kwa katibu tawala mkoani humo,atafute gari lenye uwezo wa kubeba vipaza sauti ili utekelezaji wa zoezi la kutangaza kuhusu janga la ugonjwa huo hatari liendelee kwa muda wa siku tatu mfululizo katika manispaa ya Kigoma Ujiji na wilaya zote za mkoa huo na hasa kwa vijiji vilivyojirani na mpakani.
Akithibitisha
hilo Katibu tawala wa Mkoa wa Kigoma Eng.John Ndunguru alisema mchakato huo unaanza
leo(jana) kwa mujibu wa maelekezo kutoka wizara ya afya juu ya kujihami na ugonjwa huo sanjari na viashiria kwa wahanga wa maradhi
hayo kulingana na mwingiliano wa raia ili hali tiba maalum haijathibitika.
Alibainisha kuwa wamekusudia kuyadhibiti maeneo yote ya mialo,uwanja wa ndege kwa kufanya ukaguzi kwa watu waingiao sambamba na
kutoa elimu ya ugonjwa huo na dalili zake wakatihuohuo vifaa na mavazi ya wataalam vipo tayari kwa mganga
mkuu Kigoma.



No comments:
Post a Comment