Pages

KAPIPI TV

Thursday, August 15, 2013

MAKAMPUNI YA ULINZI TABORA YALITAKA JESHI LA POLISI KUJIREKEBISHA!!!

Naibu Kamishna wa Polisi nchini  DCP Hamdani Omari Makame akizungumza na wadau  mbalimbali wa Ulinzi na Usalama mkoa wa Tabora ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani Tabora akihamasisha umuhimu wa ulinzi shirikishi jamii.
 Baadhi ya wamiliki na watendaji wa makampuni ya ulinzi mkoani Tabora wakiwa katika kikao hicho ambapo walilitaka Jeshi la Polisi kujirekebisha ikiwa ni hatua ya kuweza kufikia malengo ya kuwa na Ulinzi shirikishi Jamii ambapo walinzi na maafisa wa makampuni hayo walieleza bayana namna baadhi ya askari polisi wanavyoshindwa kutoa ushirikiano na hata kufikia hatua ya kuwanyanyasa jambo ambalo walidai kuwa linawavunja nguvu ya kushirikiana kwa dhati na askari Polisi hasa wenye vyeo vya chini.
  


Hata hivyo pamoja na wito huo uliotolewa na makampuni hayo ya Ulinzi kwa Jeshi la Polisi,Naibu kamishna wa Polisi nchini DCP Hamdani Omari Makame alisema maboeresho makubwa yanayoendelea kufanyika ndani ya Jeshi la Polisi na hivyo akawataka  wadau  wa Ulinzi na Usalama kuwa na imani na Jeshi  hilo  na kwamba  watazingatia kuwepo kwa farsafa shirikishi na vikao vya mara kwa mara hatua ambayo itasaidia kuondosha kasoro ndogondogo vinazoletwa na baadhia ya askari wachache wasio waaminifu.  



No comments: