Pages

KAPIPI TV

Thursday, August 15, 2013

JENGO LA TRA TABORA KUFANYIWA MATENGENEZO MAKUBWA KWA SHILINGI BILIONI 1.2

Jengo la ofisi za TRA mkoa wa Tabora ambalo litaanza kufanyiwa ukarabati mkubwa kuanzia sasa kwa gharama ya zaidi ya shilingi Bil.1.2 ikiwa ni hatua  muhimu ya kuboresha Jengo hilo.
Mkurugenzi wa Fedha Mamlaka ya Mapato nchini TRA Bw.Salehe Msholo akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi rasmi Jengo hilo la TRA Tabora kwa mkandarasi M/S Chengdu Shenma kutoka china ambaye atalitengeneza kwa zaidi ya miezi 12.Bw.Msholo alisema ni matengenezo makubwa yanayotarajiwa kiasi cha kuleta mabadiliko makubwa na hasa yanayolenga kufanya huduma za TRA kufanyika kwa uwazi zaidi na kuwawezesha wateja pia kuridhika na huduma hiyo.  
Meneja wa TRA mkoa wa Tabora Bw.Laurent Paul akizungumzia matarajio yao baada ya kukamilika kwa ukarabati mkubwa wa Jengo hilo linalogharimu zaidi ya shilingi Bil.1.2




No comments: