Na Esther Macha wa matukiodaima.comMbeya
KWA tukio hili jeshi
la polisi limetia aibu kubwa hakuna budi kwa jeshi hilo kufanya uchunguzi wa
kina kubaini askari wengine bandia ambao wapo katika Mikoa mbali mbali .
Ninachoweza kusema
kuhusu askari huyu feki wa kikosi cha usalama barabarani ni kwamba kazi hiyo amekuwa akiifanya kazi hiyo kwa muda
mrefu tena kwa ujasiri mkubwa lakini ujasiri huo nadhani ulitokana na kupata
nguvu kutoka sehemu fulani .
Lakini kama kweli jeshi la polisi likifanya uchunguzi wake
kwa kina yawezekana likaweza kuwabaini askari wengine wa kikosi cha
usalama barabarani ambao ni feki bila
jeshi hilo kufahamu kinachoendelea kwenye vituo vya polisi .
Ili kuweza kubaini
hilo jeshi la polisi nchini kupitia kikosi chake cha usalama barabarani lifanye
kazi yake ya kuchunguza askari mmoja baada ya mwingine kwa kuanzia kuangalia
vyeti vyake halisi na majina wanayotumia, pamoja na vyeti vya kuzaliwa kama ni
halisi.
Kwani yawezekana
hata askari waliopo kazini si askari halisi kwa utambuzi wa veti vyao hivyo
jeshi la polisi lifanye kazi hii kwa umakini ili kubaini vyeti feki kwa askari
wake.
Kwa kusema hili
naweza kusema kuwa askari huyu licha ya kufanya kazi hiyo kwa muda mrefu bila
jeshi hilo kufahamu lakini bado aliweza kufanya kazi hiyo kwa kujiamini tena
kwa kufuata taratibu zote za kazi za usalama barabarani kana kwamba amepata amesomea kazi hiyo.
Binafsi ninachoweza
kusema ni kwamba tukio hili kwa ujumla limeitia aibu jeshi la polisi kwani ni
kitu ambacho hakiwezekani trafiki huyu bandia
afanye kazi kwa muda wote huo bila kujulikana
na uongozi na hata uongozi wa juu wa jeshi hilo.
Lakini pia
kinachonishangaza ni kwamba askari huyu feki
mwenye cheo cha sajini alidiriki
hata kuwapangia kazi askari wadogo walio chini chake na hata askari hao wadogo
wanaposhindwa kuwadhibiti madereva watukutu askari hao wadogo huwapeleka kwa
askari huyo feki kwa lengo la kupigwa faini kutokana na kuogopwa na madereva kwa ujasiri wake wa kazi.
Nioanavyo kuhusu
hili ni kwamba kwa masuala ya kujeshi, hilo siyo kosa la mhusika ni kosa la
polisi wenyewe kutokuwa makini katika utendaji wao wa kazi.
Kitakachoweza
kushangaza umma ni pale askari huyu feki
kosa lake likipelelezwa kwa kasi na baadaye utasikia mara ooh kesi sijui
imefanyeje na mwisho huishia hivyo hivyo
bila wananchi kujua hatima ya huyu askari bandia .
Mimi binafsi
ninachoweza kushauri ni kwamba kama jeshi la polisi linahitaji kujisafisha
hakuna budi kwa muhusika kuchukuliwa hatua kali na hata kama kulikuwa na watu
Fulani ndani ya jeshi hilo ambao walikuwa
nyuma yake kwa lengo la kumlinda
wachukuliwe hatua.
Kwani askari huyu
feki asingeweza kuifanya kazi hii kwa ujasiri bila ya kupata ujasiri toka kwa
watu, kinachotakiwa ufanyike uchunguzi wa kina kwa askari huyu feki kwa
utaratibu nae ataweza kuongea ukweli wake halisi jinsi gani aliweza kuifanya
kazi hiyo na aliyempa ujasiri huo ni nani.
Askari feki kama
hawa wapo wengi sana hasa mikoani na njia
zilizojificha wakiendelea na kazi kama kawaida kana kwamba ni sheria
kwao kufanya kazi hiyo na hata waliofukuzwa kazi kazi katikas jeshi hilo kwa
makosa mbali mbali pia wamo katika idadi hiyo yta askari feki .
Ili kuona jeshi hilo linaondokana aibu hiyo pia
lijaribu kuangalia hata askari wake ambao walifukuzwa kazi kwa makosa mbali
mbali ndani ya jeshi hilo ,kwani nao
wanaweza kuwa sababu ya kulichafua jeshi hilo.
Kitu kingine ambacho
naweza kusema ni kuhusu hawa askari kanzu wa jeshi la polisi waliopo katika
mikoa mbali mbali nchini ,hawa nao jeshi la polisi inabidi lifanye kazi yake ya
kiuchunguzi kubaini nao kama ni askari halisi
maana hawa nao wamekuwa wakichanganya wananchi .
Nadhani kuanzia sasa
uongozi wa juu wa jeshi hilo uwe na utaratibu maalum kwa askari wake hasa wa kikosi cha usalama barabarani na
askari kanzu kuwa na vitambulisho maalum kwani yawezekana hata kitengo hiki cha
askari kanzu pia kikawa na watu wa namna hiyo bila jeshi la polisi kufahamu.
Nionavyo kuhusu hili
si jambo la kupuuza kwa ngazi za juu za jeshi la polisi ili kuweza kunusuru jeshi hilo katika kashfa
mbaya na hata kurudisha imani kwa wananchi ambao wamekuwa wakiamini kazi kubwa
ya jeshi hilo.
Tukio la askari huyu bandia mwenye cheo cha sajini, (jina halikupatikana)
alikamatwa na Polisi akiwa 'kazini' maeneo ya Tabata Kinyerezi akiwa amevaa
sare mpya ya Askari wa Usalama Barabarani, akiwa na kikoti cha kuakisi mwanga
na kofia nyeupe.
Pia trafiki
huyo alikuwa na jalada pamoja na kitabu cha kutoza faini (Notification) kwa
madereva wanaopatikana na makosa ya kukiuka sheria za usalama barabarani.
Katika
taarifa ya gazeti hili la majira lilishuhudia trafiki huyo feki akiwa
amekamatwa na Polisi na kisha kufikishwa Kituo Kikuu cha Polisi Kati, huku
akijifanya amepoteza fahamu.
Ushauri
wangu kwa jeshi la polisi wajiangalie vizuri katika utendaji wao wa kazi kwani
wananchi wanazidi kukosa imani na utendaji wa kazi wa jeshi hilo ,kitendo cha mpaka raia kuvaa
sare za jeshi hilo kwa muda mrefu bila hata jeshi hili kutambua kitu gani
kinaendelea ni aibu kubwa kwa jeshi.
Kama jeshi
la polisi wanatakiwa kuanza kujiangalia upya na kujitafakari kwa haya matendo
mabaya yaliyopo mbele yao na kujisafisha mbele
ya wananchi ambao wanawaongoza.
No comments:
Post a Comment