Pages

KAPIPI TV

Thursday, August 2, 2012

VIONGOZI WA DINI,VYAMA VYA SIASA TABORA WAPATIWA SEMINA KUHUSU SENSA YA WATU NA MAKAZI

 Sheikh mkuu wa mkoa wa Tabora,Shaaban Salum akizungumza na baadhi ya viongozi wa dini na vyama vya siasa wakati wa mkutano wa Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012,Sheikh Shaaban Salum aliwaasa kuepukana na mitandao inayodai kutaja idadi ya Wakristo,Waislam,na Wasiokuwa na dini jambo ambalo limeonekana ni sehemu ya kusababisha mifarakano kwa jamii ya Kitanzania
 Mchungaji wa Kanisa la Agape Mwanzaroad mjini Tabora,Elias Mbagata akitoa maoni yake kuhusu zoezi la Sensa ya watu na makazi linalotarajiwa kufanyika hivi karibuni hapa nchini,ni katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Tabora. 
 Mkuu wa mkoa wa Tabora Fatma Mwassa akifungua mkutano huo wa Sensa ya watu na makazi uliokuwa ukiwahusisha baadhi ya viongozi wa Dini madhehebu mbalimbali na vyama vya Siasa.
 Baadhi ya viongozi wa dini wakiwa wanasikiliza kwa makini katika mkutano huo wa Sensa ya watu na makazi uliofanyika katika ukumbi  wa Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Tabora.
 Mkuu wa mkoa wa Tabora Fatma Mwassa akiwa na baadhi ya viongozi wa dini na vyama vya siasa katika mkutano huo wa Sensa ya watu na makazi.
 Viongozi wa dini ya Kikristo wakiwa katika mkutano huo wa Sensa ya watu na makazi.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo wa Sensa ya watu na makazi wakisikiliza mada mbalimbali zinazohusu mchakato wa kuhesabu watu na namna zoezi zima litakavyoendeshwa.

No comments: