Meneja wa Tanesco mkoa wa Tabora,Injinia Mahende Mugaya Mugaya, |
TANESCO mkoa wa Tabora ni moja kati ya mikoa iliyo chini ya idara ya
usambazaji na huduma za wateja ya Shirika la umeme la Tanzania.
Injinia Mahende Mugaya Mugaya,ni meneja wa shirika la umeme Tanesco,
mkoa wa Tabora,alifanya mazungumzo na mwandishi wa makala hii na
kuweka mipango utendaji na malengo ya shirika hilo kwa situ zijazo.
Injinia Mugaya anafafanua kuwa shirika lina jukumu la kuhakikisha
kwamba maeneo yote yaliyo mkoa wa Tabora yanahudumiwa vyema kulingana
na mkataba wa huduma kwa mteja uliopo kati ya kampuni na wateja na
Makro mkuu ya wilaya zote yanapata huduma za uhakika.
Meneja huyo anabainisha kuwa Tanesco mkoa wa Tabora inajishughulisha
na huduma za usambazaji wa umeme kwa wateja wa mkoa wa Tabora, huduma
zinazotolewa chini ya usambazaji ni kupokea maombi ya wateja tarajiwa
na kuyashughulikia, kuunganisha umeme kwa wateja waliokwisha
lipia,kuchukua usomaji na mita na utayarishaji wa Ankara za umeme.
Anafafanua zaidi kuwa huduma nyingine inayofanyika ni ukusanyaji wa
Mapato toka kwa wateja wetu, ukaguzi kubaini udanganyifu na wizi wa
umeme kwa wateja wasio waadilifu na pia usalama wa mifumo ya umeme
ndani ya majengo.
Anaongeza kuwa shirika hilo, linashughulika na huduma ya dharura ili
kuwarejeshea wateja umeme pale panapokuwa na tatizo la katizo la umeme
bila kutarajia.
Anaeleza zaidi kwamba kazi nyingine ni kuifanyia matengenezo mifumo ya
usambazaji umeme pamoja na ile ya usafirishaji na mwisho kabisa ni
kutoa elimu kwa wateja wetu kuhusu huduma tunazozitoa ili kutoa uelewa
kwa wateja kujua haki na wajibu wao.
Alisema kuwa hadi mwezi juni 30 mwaka 2012 mkoa una jumla ya wateja
wapatao 22,830, kati ya wateja wote, wale watumiao mita za LUKU
wanafikia 19,566 na wale wanaotumia mita za malipo baadaye wapo 3,264.
Injiania Mugaya anasema kati yao wateja wakubwa wapo 32 (wale
wanaotumia zaidi ya Unit 7,500 kwa mwezi), ambapo lengo la Shirika ni
kuhakikisha wateja wote wa majumbani na biashara ndogo ndogo
wanafungiwa mita za LUKU.
Malengo waliyojiwekea 2012.
Injinia Mugaya anazungumzia malengo aliyojiwekea katika kipindi cha
bajeti ya mwaka 2012, (Kalenda ya Shirika inaanza January hadi Desemba
), Shirika Mkoa wa Tabora tumejiwekea malengo kadhaa.
Anafafanua kuwa shirika limeweka malengo hayo ambayo ni kuunganisha
wateja wapya wasiopungua 2,750, kuunganishiwa wateja wapya ndani ya
siku 30 tangu mteja kukamilisha malipo na kupunguza idadi ya Ankara
zisizokuwa safi hadi kufikia asilimia 0.1 ya Ankara zote.
Aidha meneja huyo anasema malengo mengine ni ukusanyaji mapato kwa
asilimia 100 kwa bili za kila mwezi pamoja na ukusanyaji wa deni la
nyuma kwa asilimia 50 na kuimarisha kitengo cha huduma za dharura ili
kuondoa kero kwa wateja wetu.
Anaongeza kuwa malengo mengine ni kuwasimamia vyema Makandarasi ili
kumaliza miradi yenye ufadhili wa Wakala wa Umeme vijijini( REA )ndani
ya mwaka huu wa 2012, kuimarisha ukaguzi kwa wateja ili kupunguza
matukio ya wizi wa umeme yanayofanywa na wateja wasio waaminifu hivyo
kudhulumu mapato ya Shirika.
‘‘Malengo mengine ni kupunguza matukio ya wateja kuombwa rushwa na
wafanyakazi wasio waadilifu.....na kupunguza ajali na kuimarisha Afya
na Usalama kwa wafanyakazi na raia kwa ujumla.” Alisema.
Utendaji hadi nusu ya mwaka januari hadi juni na matokeo yake.
Akizungumzia utendaji katika kipindi cha mwezi januari januari hadi
mwezi juni, Injinia Mugaya anafafanua kuwa utaratibu wa upimaji
uliwekwa wazi kwa wateja wote ili kuandoa usumbufu usio wa lazima.
Aidha anaongeza kuwa mkoa wa Tabora umefanikiwa kuwaunganishia wateja
wapya wapatao 706 ikiwa ni asilimia 26 ya lengo la mwaka na
upatikanaji wa vifaa vya kuungia wateja hasa mita haukuwa mzuri kwa
kipindi cha January hadi April 2012.
Alisema hata hivyo kuanzia mwisho wa mwezi wa tano upatikanaji wa
vifaa umeimarika na kasi ya uunganishaji umeme kwa wateja waliopia
imeongezeka na hadi kufikia kwezi juni 30 mwaka 2012 mkoa mzima
ulikuwa na wateja 81 tu waliolipia umeme na wanasubiri kuungiwa.
Alisema wote hawa malipo yao yamefanyika ndani ya mwezi wa sita ambapo
nia ni kufikisha lengo la wateja 2750 na tunataraji kulifikia
kulingana na kuimarika kwa upatikanaji wa vifaa vya ujenzi.
‘‘Napenda kuwataarifu wateja wetu kwamba shirika limetenga fedha kwa
ajili ya kusogeza huduma ya umeme kwa wateja kwa kujenga mifumo ya
umeme katika maeneo mbalimbali mkoani Tabora.
Injinia Mugaya alibainisha maeneo hayo kuwa manispaa ya Tabora ni eneo
la Mwinyi Skanda, Mwinyi Simbawene, Ipuli D na Luwanzari.
Aidha maeneo mengine ni katika wilaya ya Igunga katika maeneo ya
Hanihani, Magereza masanga na Nkokoto na wilaya ya Sikonge katika
maeneo ya Pangale,Usega, Tutuo na Uranga.
Aidha naongeza kwa upande wa wilaya ya Urambo maeneo hayo ni
Kichangani, New stand, machinjioni na eneo la barabara kuelekea
Ulyankulu na wilaya ya Niega ni Ifukeli, Uswiru, Kazaroho,Kikongo na
Ipilili.
Usomaji wa mita
Injinia Mugaya alizungumzia usomaji wa mita za umeme na kusema kuwa
chini ya uongozi wake, wameimarisha usimamizi wa usomaji mita na
kufanikiwa kupunguza Ankara zisizo sahihi kutoka asilimia sifuri nukta
tano 0.5, ya Disemba 2011 hadi asilimia sufuri nukta tatu 0.3,ya mwezi
June, 2012.
Alisema lengo ni kuondokana na tatizo hili kabisa, ambapo mkoa wa
Tabora umeweza kuuza Unit za Umeme zipatazo 39,131,548 zenye thamani
ya sh 6,535,912,194, kwa mita za mkopo ambazo wateja hulipia baada ya
matumizi.
Aidha anafafanua zaidi kuwa makusanyo kutokana na mauzo hayo yamekuwa
sh bilioni 6,706,359,062. ambayo ni sawa na asilimia mia moja, na
tatu 103 ya mauzo na makusanyo yapo juu ya mauzo kwa vile mkoa
unafanya jitihada ya kukusanya malimbikizo ya madeni ya nyuma.
‘‘Kimsingi ziada iliyokusanywa ni asilimia 30 ya deni lote
lililokuwepo hadi Disemba 2011….. ni matarajio yetu tutavuka lengo
tulilojiwekea la kukusanya zaidi ya 50 ya deni husika.” Alisema.
Mauzo ya uniti kupitia mita za LUKU.
Injinia Mugada alizungumzia uuzaji wa uniti kupitia mita za LUKU Nna
kubainisha kuwa, katika mfumo wa mita za malipo kabla, maarufu kama
LUKU, tumeweza kuuza unit zipatazo 10,907,159 zilizotuingizia kiasi
cha sh bilioni 2,655,222,759.
Kitengo cha urejeshaji umeme.
Meneja huyo alisema kuwa kitengo cha dharura ambacho hushugulika
na kurejesha umeme kwa wateja waliokosa umeme kutokana na matatizo
mbalimbali ya kiufundi kiliimarishwa.
Alisema kuwa katika suala la upokeaji wa simu toka wa wateja
umeboreka na vile vile wateja hutembelewa kwa wastani wa ndani ya
masaa kumi na mbili (12), tangu kutoa taarifa na huduma ya umeme
kurejeshwa.
Anaongeza mkoa unatekeleza miradi ya Umeme Vijijini chini ya ufadhili
wa Mamlaka ya Umeme Vijijini (REA), ambapo miradi hiyo imelenga
kupeleka Umeme katika kata ya Bukene Wilayani Niega mkoani Tabora.
Injinia Mugada alisema vijiji vilivyopo njiani kati ya Nzega Mjini, na
Bukene, navyo vitafaidika na mradi huu,ambapo vijiji hivyo ni Ijanija,
Busasu na Itobo, vingine ni njia panda na Itonjanda.
‘‘Mradi huu vile vile utahusika na usambazaji Umeme katika kata ya
Ndala ambao pia ipo wilayani Niega…..na vijiji vitakavyonufaika ni
Itiro, Uwigu, Mwanhala na Ngukumo. Vingine ni Nkiniziwa, Busondo,
Utunguru, Puge na Kampala.” Alisema.
Alibainisha kuwa miradi hii inataraji kuunganisha umeme kwa wateja
wapatao 656, ambapo kwa upande wa wilaya ya Urambo nayo inao mradi
wenye ufadhili wa REA, ambao unataraji kufikisha umme katika maeneo
kadhaa.
Alitaja maeneo hayo kuwa ni Kalemela A na B, Mabatini, Vumilia, Usoke
Mlimani na kuiboresha njia ya Kaliua kuwa Njia tatu badala ya moja,na
Miradi hii inafanywa na kampuni ya ukandarasi Umeme iitwayo NAMIS
CORPORATE LTD, ya jijini Dar es salaam.
Anaeleza zaidi kuwa hadi sasa tumeisha unganisha wateja wapatao 56,
katika eneo la Bukene, na wateja wapatao 26 katika wilaya ya
Urambo ambapo mradi huu unatarajiwa kukamilika kabla ya mwezi wa kumi
na mbili 2012.
Watumiaji wa umeme bila kulipia.
Injinia Mugaya alifafanua zaidi juu ya watumaji wa umeme wasio
waaminifu na kusema kuwa shirika la Tanesco Tabora, linaendesha zoezi
la ukaguzi ili kuwabaini wale wanaotumia umeme bila kulipia aidha kwa
kuchezea mita au kutopitisha umeme kwenye mita.
Alisema kwa kipindi cha Januari hadi June 2012, tuliweza kuwatembelea
kwa ajili ya ukaguzi wateja wapatao 2,494,ambapo kati yao wateja 21,
waligundulika kuliibia shirika kwa kutumia umeme bila kupita kwenye
mita.
Aliongeza kuwa kati yao manispaa ya Tabora, walikuwa 5, wilaya ya
Nzega 5, wilaya ya Sikonge 8, na wilaya ya Igunga 3 na kiasi cha sh
milioni 9,645,315.45 zilikusanywa kama mapato yaliyopotea ,na sh
milioni 5,824,197. zimekusanywa kama faini na gharama za ukaguzi.
Alisema zoezi hili ni zoezi endelevu na kuanzia mwezi June 2012,
shirika la Tanesco Tabora limeazimia kuwafikisha kwenye vyombo vya
sheria wale wote watakaopatikana wanaiba umeme.
‘‘Iwapo wapo wafanyakazi wenzetu wataogundulika kusaidia katika wizi
hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yao mara moja......na katika
hili tuna maana halisi, na nitoe taarifa kwamba tumewaachisha kazi
wafanyakazi wawili katika wilaya ya Sikonge baada kuridhihirika bila
shaka waliwasaidia wateja kuiba umeme.” Alisema.
Hata hivyo meneja huyo aliongeza na kutoa wito kwa kuwataarifu wateja
wote wa umeme na wanachi wa mkoa wa Tabora, kwa ujumla kwamba shirika
lina dhamira kubwa ya kuboresha huduma zake kama ilivyoainishwa kwenye
mkataba wa huduma bora kwa wateja.
Alisema kwa kufafanua zaidi kuwa mkataba ambao umepata baraka za
mamlaka ya uthibiti wa Nishati na Maji (EWURA). Ili kuboresha huduma
zetu tunahitaji ushirikiano mkubwa sana wa wateja na wananchi kwa
jumla.
Alieleza kuwa ushikiano huu ni pamoja na kutuletea taarifa zinazohusu
uhujumu wa miundo mbinu ya umeme, wafanyakazi wasio waadilifu
wanaowasumbua wateja katika kutoa huduma na watumishi wa shirika
kuwaomba rushwa au kuwazungusha bila sababu za msingi, na wale
wanaotumia umeme kwa wizi na wanaokwepa kulipa madeni yao ya umeme.
Aidha alisema kuwa wananchi wote kwa sasa shirika lina mita za kutosha
kuwaunganishia wateja wote watakaolipia kupata huduma ya umeme,na
wateja wote wenye mita zilizosimama tafadhali watoe taarifa katika
ofisi zetu mara moja.
Pia wale ambao wanajua wamechezea mita kwa nia ya kuliibia
shirika,wajisalimishe wenyewe zetu ili kukwepa mkono wa sheria
kuwafika.
No comments:
Post a Comment