Pages

KAPIPI TV

Friday, August 24, 2012

SITTA AWASHAURI WANA-CCM KUHESHIMU MAAMUZI YA MAHAKAMA

Na Lucas Raphael,Tabora

WAZIRI WA Ushirikiano wa Africa mashariki na mbunge  wa jimbo la Urambo mkoani Tabora (CCM)  Samwel Sitta amewataka wana-CCM kuheshimu maamuzi yaliyotolewa na mahamaka kuu kanda ya Tabora ya kutengua ubunge jimbo la Igunga.

Sitta alisema kwamba mahakama imefanya kazi yake kwa kutoa uamuzi huo kwani hiyo ndio ilikuwa uamuzi ila alitaka chama cha mapinduzi kujipanga upya kama itakata Rufaa ama laa

Aliyasema hayo jana mjini Tabora wakati akikabidhi vifaambalimbali ikiwemo  Kompyuta mbili na printa zake kwa Vijana wakatoliki (VIWAWA) vyenye thamani ya shilingi milioni mbili na nusu ambazo aliwataka kuzitumia kwa makini na uadilifu mkubwa ili viweze kudumu.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo alisema, kwa kuwa Mahakama inamamlaka yake kisheria wana CCM hawana budi kuyaheshimu maamuzi hayo kwani mahakama imefanya kazi yake inavyotakikana.

“Kama kunamtu anaona hukumu hiyo haikutenda haki anaweza kwenda mahakamani kukata rufaa, lakini mimi nashauri nivyema tujipange upya tuingie ulingoni” alisema Sitta.

“Hapa mimi sina maoni juu ya jambo hilo bali chamsingi ni vyema tukakaa kutafakali yaliyotokea huko Igunga, ili basi tukiona inafaa kukata rufaa sawa, nakama tuingie ulingoni yote ni sawa” alisisitiza Bw. Sitta.

Kuhusu ufisadi ,Sitta ambaye pia ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki alisema yeye kama kiongozi wa serikali ni vema akafuata maadili ili hata anaahidi kutoa mchango wake kwa watu hawezi kutoa kwa harakaharaka, kwani maadili yanaweza kumbana.

“Unajua sisi viongozi wa Serikali pesa zetu ni lazima uzitoe polepole ukifanya haraka utaitwa fisadi”alisema waziri Sitta.

Kwa upande wake mkuu wa itifaki wa VIWAWA jimbo kuu la kanisa katoliki ,John Pinini alisema kwamba Ni kiongozi wa kuigwa, na kuwaomba viongozi wengine wa serikalini kuwa na moyo kama huo kwa kumtolea Mungu.

Sitta ametoa kauli hiyo siku mbili baada ya  Mahakama Kuu ya kanda ya Tabora kutengua ushindi wa mbunge wa  jimbo la Igunga Dkt,Peter Dalali Kafumu, kufuatia mahakama hiyo kukubaliana na hoja za upande wa mlalamikaji dhidi ya CCM Joseph Kashindye kwamba uchaguzi huo uligubikwa na vitendo vya rushwa.

Ilielezwa kwamba Katika moja ya mikutano ya kampeni ya uchaguzi huo mdogo wa jimbo la Igunga uliofanyika mwaka jana, Rage alipita mitaani huku akiwatangazia wananchi kuwa mgombea ubunge wa Chadema amejitoa hivyo wasijisumbue kumpigia kura na badala yake wamchague mgombea wa CCM.

No comments: