Mstahiki
Meya wa manispaa ya Ilala Bw.Jerry Silaa akimkabidhi fomu za
kugombea nafasi ya ujumbe wa UVCCM-NEC kwa katibu wa UVCCM mkoani Mwanza Bw
Elias Mpanda, jana katika ofisi za CCM Jijini Mwanza.
Mstahiki
meya wa Manispaa ya Ilala Bw Jerry Silaa anagombea nafasi ya ujumbe wa
UVCCM-NEC ngazi ya taifa.
Katika kauli yake Mstahiki meya Bw.Silaa aliweka wazi nia yake ya kutaka
kuwawakilisha vema vijana wa kitanzania kwenye UVCCM-NEC na huku akiwaasa
vijana wengine nchini kushiriki kwenye mchakato huo na kwamba
yuko tayari kufanya kazi kokote nchini kwa maslahi ya wananchi,
Katika hatua nyingine Mstahiki
meya huyo alitumia fursa hiyo kuwaasa viongozi wa kada mbalimbali nchini kuwajibika na kutimiza ahadi zao
walizozitoa kwa wananchi huku wakiweka mbele maslahi ya taifa na sio yao
binafsi.
|
No comments:
Post a Comment