Pages

KAPIPI TV

Tuesday, August 7, 2012

MBIO ZA KUWANIA UONGOZI NDANI YA JUMUIYA ZA CCM ZAANZA TABORA

Joseph Michael Ngulumwa
Na Hastin Liumba,Tabora

HEKIMA, UZALENDO NA BUSARA NI KIELELEZO CHA YA KIONGOZI BORA NA MAKINI.
UZALENDO,hekima na busara ndivyo vinayonisukuma kuchukua fomu ya
kuomba kugombea nafasi ya mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi mkoa wa
Tabora.

Joseph  Michael Ngulumwa ,alitoa kauli hiyo wakati alipokuwa akifanya
mahojiano na mwandishi wa makala hii ofisi za CCM mkoani Tabora.

Ngulumwa  ni mtumishi idara ya madini,mkoa wa Tabora,akiwa ni mtaalamu
wa miamba na madini.

Ngulumwa alisema kuwa amefikia hatua hiyo baada ya kuona ana sifa ya
kuomba,nafasi ya mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi mkoa wa Tabora na
hasa uzoefu mkubwa alionao ndani ya chama na jumuiya zake.

Alisema kiongozi yoyote anapaswa kuwa na uzalendo,hekima,busara na
elimu kwani vigezo hivyo kwake yeye vimesheheni,na ana amani ya kuwa
vigezo hivyo vikitawala vichwani mwa viongozi wetu, tutakuwa na taifa
linalosonga mbele kiuchumi,kisiasa na kiutamaduni.

Ngulumwa alichukua fomu mwezi agosti 2,mwaka huu kuomba kugombea
nafasi ya mwenyekiti wa jumuiya ya WAZAZI, mkoa wa Tabora, katika
uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mapema mwezi septemba mwaka huu.

Akiwa mwenyekiti mstaafu wa jumuiya ya umoja wa vijana,(UVCCM),alisema
hatua ya kuchukua fomu, hasa ni kutokana na jumuiya hiyo kuonekana
kama haiko hai, na kwamba kulingana na uzoefu alioupata akiwa jumuiya
hiyo kwa zaidi miaka 10 atafanikiwa kuiamsha jumuiya ya wazazi mkoani
Tabora.

Aidha alisema ameamua kuchukua fomu pia ni kutaka jumuiya hiyo
iondokane na hali ya utegemezi hali ambayo itajenga heshima ya jumuiya
na chama kwa ujumla.

Aidha alisema ilani ya uchaguzi inaelekeza utekelezaji wa ilani ni
hivyo ana nafasi kubwa ya kuweza kuisimamia kiutamaduni,kisiasa na
kijamii na bila kusahau sekta michezo,hivyo ni nafasi yake kuunganisha
jamii kushiriki katika michezo kwani michezo licha ya kuwa ni sehemu
ya kujiweka vyema kiafya,pia ni ajira.

Anasema jamii ikishirikishwa vyema kwenye miradi ya maendeleo,michezo
ni dhahiri maendeleo husika yatafikiwa kwa kiwango kikubwa na
kinachotakiwa ni kuthubutu tu.

Endapo atachaguliwa atafanya nini.

Aidha alisema endapo atafanikiwa kupata nafasi ya kuwa mwenyekiti wa
jumuiya ya wazazi mkoa wa Tabora,atashirikiana na viongozi wenzake
kubuni na kuanzisha miradi kadhaa ikiwemo ujenzi wa sekondari lakini
mwanzo atafanya ni kutafuta ardhi  kubwa kwa ajili ya ujenzi wa
sekondari hiyo na miradi mingine.

Ngulumwa anafafanua kuwa elimu kwa sasa ni jambo la kutiliwa mkazo
kama mwenyekiti wa wazazi endapo nitachaguliwa kipaumbele hicho kwake
ni muhimu sana hasa ikizingatiwa elimu, itasaidia katika kuingia
kwenye ushindani wa soko la ajira katika Afrika Mashariki na Dunia kwa
ujumla.

Alisema mkoa wa Tabora katika suala la elimu bado uko nyuma sana hivyo
ni nafasi yake endapo atachaguliwa kuhakikisha sekta ya elimu inapiga
hatua haraka.

Alisema kuwa miradi mingine anayofikiria ni ujenzi wa vibanda
vitakavyokodishwa kwa watu kwa stahili ya kupangisha na kukusanya
kodi.

‘‘Nikiwa mtalaamu wa madini itakuwa ni nafasi yangu kuangalia
uwezekano wa maeneo yenye madini na kutengeneza utaratibu wa kuweza
kumiliki kisheria kama wachimbaji wadogo.” Alisema


‘‘Niseme wazi tu kuwa mkoa wa Tabora una fursa nyingi lakini
hazitumiki......lakini  zikitumika vyema mkoa utabaidilika kwa kasi
kubwa.” Alisema

Anazungumziaje uchaguzi katika jumuiya ya wazazi.

Ngulumwa anazungumzia uchaguzi huo na kusema kuwa, katika uchaguzi huo
anapendelea uwe wa haki pasipo matumizi ya rushwa kwani hatutaweza
kuwa na uongozi wa kiadilifu endapo rushwa itakuwa ni kigezo cha
mgombea kuungwa mkono.

Alisema tunapaswa kutafuta viongozi wenye uzalendo zaidi ili kujenga
taifa lenye watu makini na waadilifu ili kizazi kijacho kirithi jamii
iliyostaarabika.

Mwenyekiti huyo mstaafu wa (UVCCM), mkoa wa Tabora anasema kwa (CCM),
inayojengwa sasa na jumuiya zake inapinga na kukemea vikali matumizi
ya rushwa katika chaguzi mbalimbali.

Alisema upepo uliopo ndani ya bunge ambao unazungumzia matendo ya
rushwa kutopewa nafasi katika kutekeleza majukumu ya kila siku,ni
dhahiri viongozi wetu sasa wameona mbali madhara ya rushwa.

Alisema wanachama wenye sifa za uongozi ndani ya (CCM), wapo isipokuwa
wanaminywa na baadhi ya wachache wanaotumia na kuendekeza matendo ya
rushwa katika chaguzi.

Aliongeza kuwa akichaguliwa bila kujali itikadi atashirikiana na jamii
kwa kukemea mambo yote yatakayokuwa yanaelekea kuvuruga chama,jumuiya
na taifa.

Historia yake kwa ufupi.

Joseph Ngulumwa Michael alizaliwa mwezi januari 27 mwaka 1974,katika
wilaya ya Nzega,mkoa wa Tabora.

Uzoefu ndani ya chama.

Anasema ana uzoefu mkubwa ndani ya chama ambapo alijiunga na (CCM),
toka mwaka 1990 akiwa kidato cha nne katika shule ya sekondari Tabora
wavulana.

Alisema licha ya kushika nyadhifa kadhaa ndani ya chama na jumuiya ya
(UVCCM) ,pia alichaguliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1998 kuwa mjumbe wa
kamati ya utekelezaji ya mkoa wa Tabora nafasi aliyodumu nayo hadi
mwaka 2004 ndipo alipochaguliwa kuwa mwenyekiti wa (UVCCM) mkoa wa
Tabora.

Ngulumwa anaongeza nafasi ya mwenyekiti wa jumuiya ya umoja wa vijana
(UVCCM), alidumu nayo kwa kipindi cha miaka mitano toka mwaka 2004
hadi mwaka 2008, na kwa sasa ni mjumbe wa baraza kuu wa (UVCCM), mkoa
wa Tabora.

Alisema hadi sasa ana kadi za jumuiya zote tatu, ambapo namba ya kadi
ya WAZAZI ni kadi yake ni 013883 ya mwaka 2005, CCM ya zamani ni namba
934049 ya mwaka 1990,ambapo mpya ya sasa ni 423150 na UVCCM ni 111429
ambayo ni mpya na ya zamani ni namba 204750 ya mwaka 1990.

Elimu yake

Ngulumwa anazungumzia elimu yake na kusema kuwa, baada ya kuhitimu
elimu ya sekondari kidato cha nne katika sekondari ya  Tabora
wavulana, alijiunga na chuo cha madini mkoani Dodoma mwaka 1991 hadi
mwaka 1993.

Alisema alijiunga na jeshi la kujenga taifa,(JKT),Maramba (operesheni
vyama vingi) wilaya ya Lushoto mkoani Tanga mwaka 1993 na kuhitimu
mwaka 1994.

Aidha anasema katika kipindi hicho aliamua kujiendeleza na masomo ya
kidato cha sita katika chuo cha walimu TTC Tabora mwaka 2001na baadaye
alijiunga na chuo kikuu huria na khitimu masomo yake na kutunukiwa
cheti cha stashahada jumuiya ya madola katika shughuli za vijana, hiyo
ikiwa mwaka 2002 hadi 2004.

Aidha aliongeza kuwa baada ya kumaliza mafunzo yake yake (JKT),
aliajiriwa katika halmashauri wilaya ya Nzega,mkoani Tabora kama
mtendaji wa kata mwaka 1994 hadi mwaka 2004.

Alisema akiwa afisa mtendaji wa kata aliwahi kufanya kazi katika kata
za Itobo,Bukene na Semembela zote za wilaya ya Nzega.

Nafasi ya mwenyekiti wa WAZAZI mkoa wa Tabora iko wazi kwa sasa,lakini
kabla ya hapo ilikuwa ikishikiliwa na mbunge wa jimbo la Tabora mjini,
Alhaj Ismail Aden Rage, ambaye ameshatangaza kuwa hatogombea tena
nafasi hiyo kutokana na kutingwa na majukumu mengi.

Anamalizia kwa kusema kuwa endapo akichaguliwa katika nafasi ya
mwenyekiti wa wazazi mkoa wa Tabora kikubwa atakachofanya ni kumaliza
tofauti za makundi kwani zimekuwa na athari kubwa sana kwa chama.

‘‘Hakuna ubishi hebu jaribu kuangalia siasa za makundi jinsi
zinavyokuwa mwiba na kikwazo cha kufikiwa kwa
maendeleo......nisingependa kuyapa nafasi kubwa kwenye uongozi wangu
endapo nitachaguliwa kuwa mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi mkoa wa
Tabora.” Aliongeza.

No comments: