Mkuu wa wilaya ya Uyui Lucy Mayenga akisoma hotuba wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Sensa ya watu na makazi kwa makarani zaidi ya 713 wa wilaya ya Uyui wanaotarajiwa kuendesha zoezi hilo ifikapo tarehe 26 Agost 2012.
Baadhi ya makarani wa Sensa ya watu na makazi wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Uyui Bi.Lucy Mayenga wakati akifungua mafunzo ya Sensa.
Na Mwandishi Wetu Tabora.
Na Mwandishi Wetu Tabora.
Mkuu wa wilaya ya Uyui mkoani Tabora Bi.Lucy Mayenga amewataka makarani wa Sensa ya watu na makazi wilayani humo kufanya zoezi hilo kwa makini ili kuwezesha Serikali kupata takwimu sahihi zitakazosaidia kupanga mipango yake katika kuwahudumia wananchi wake.
Bi.Lucy alikuwa akiongea na makarani wa Sensa ya watu na makazi wa wilaya hiyo wakati akifungua mafunzo ya uendeshaji wa zoezi la Sensa ya watu na makazi yanayofanyika katika Shule za Sekondari za Kazima na Milambo Tabora mjini.
Ili serikali iweze kutoa huduma kwa uhakika kwa wananchi wake mkuu huyo wa wilaya alisema takwimu sahihi za idadi ya watu ndio nguzo pekee itakayosaidia kufikia mipango na malengo ya Serikali iliyojiwekea na huku akipigia mfano zaidi suala la mgawanyo wa rasilimali katika sekta mbalimbali ikiwemo afya,kilimo na hata ajira kwa vijana jambo ambalo limekuwa ni changamoto kubwa.
Aidha Bi.Lucy ambaye pia ni mbunge wa vitimaalum alitumia fursa hiyo kuwataka makarani hao kufanya kazi hiyo kwa uzalendo huku wakitanguliza mbele maslahi ya Taifa.
Jumla ya makarani 713 ndio walioteuliwa kuendesha zoezi la Sensa ya watu na makazi kwa wilaya ya Uyui.
No comments:
Post a Comment